Dumuzi mkubwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Masahihisho
Sahihisho
Mstari 35:
 
==Mwenendo==
Dumuzi mkubwa ni msumbufu wa hatari wa mahindi na viazi vikavu vya muhogo zinazohifadhiwa, na atashambulia mahindi shambani kabla ya uvuno. Majaribio ja kukuza spishi hiyo kwenye [[kunde]], [[maharagwe]], [[kakao]], [[buni (tunda)|buni]] na [[mchele]] usiokobolewa katika [[maabara]] hayakufanikiwa, ingawa ukuaji unawezekana kwenye aina nyororo za [[ngano]] na ulaji wa wapevu unaweza kuharibu bidhaa hizi nyingine.
 
Dumuzi mkubwa hutenda kama msumbufu wa kawaida wa mahindi yaliyohifadhiwa shambani. [[Punje]] nzima hushambuliwa kwenye [[bunzi (muhindi)|mabunzi]] kabla na baada ya kuvuna. Pia ni msumbufu wa mahogo yaliyohifadhiwa shambani, haswa [[chipsi]] za muhogo. Wapevu hutoboa vyakula vingi na vitu vingine vikiwemo [[kuni]], [[mwanzi]], [[plastiki]] na [[sabuni]]. Idadi kubwa za dumuzi wakubwa hutokea katika [[mazingira]] ya asilia na wamerekodiwa juu ya spishi kadhaa za [[mti|miti]] huko Amerika ya Kati (Rees et al., 1990; Ramirez-Martinez et al., 1994) na Afrika (Nang'ayo et al., 1993, 2002; Nansen et al., 2004) katika visa vingine wakioanishwa na [[mbawakawa vipapasio-virefu]] wanaotoa [[mviringo|miviringo]] ya [[gome]] kutoka [[tawi|vitawi]] (Borgemeister et al., 1998).