Dumuzi mkubwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Nyongeza matini kuhusu udhibiti
dNo edit summary
 
Mstari 23:
 
==Maelezo==
Dumuzi mkubwa ana urefu wa [[mm]] 3-4.5 kulinganisha na urefu wa mm 2-3 katika dumuzi mdogo. Mpevu ana umbo la [[mcheduara]] la kawaida la Bostrichidae na ncha ya nyuma inayoonekana kama imekatwa. [[Kichwa]] kimefichwa kutoka juu chini ya [[pronoto]]. Uso wa [[mwili]] una vijishimo na chembe nyingi ndogo ndogo kama [[sugu]] ([[kinundu|vinundu]]). [[Kipapasio|Vipapasio]] vina [[pingili]] 10 na vina [[rungu|kirungu]] chenye pingili tatu, ambazo ile ya mwisho ni pana sawa au zaidi kuliko pingili zilizotangulia. 'Shina' la kipapasio ni jembamba na limefunikwa kwa [[nywele]] ndefu<ref>[https://keys.lucidcentral.org/keys/v3/eafrinet/maize_pests/key/maize_pests/Media/Html/Prostephanus_truncatus_Horn_-_Larger_Grain_Borer_%28LGB%29.htm] Dumuzi mkubwa kwenye EAFRINET</ref><ref name="CABI">[https://www.cabi.org/isc/datasheet/44524] Dumuzi mkubwa kwenye CABI</ref>.
 
[[Buu|Mabuu]] ni weupe na wororo na wamefunikwa kwa nywele habahaba. Pande zao ni [[sambamba]], yaani hazipunguzi. [[Mguu|Miguu]] ni mifupi na kidonge cha kichwa ni kidogo kulinganisha na saizi ya mwili<ref name="CABI" />.