Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Redirecting to IAEA
 
No edit summary
Mstari 1:
[[Image:Tuzo Nobel.png|left|80px]]
#redirect [[IAEA]]
[[Image:Flag of IAEA.svg|thumb|right|Bendera ya IAEA]]
[[Image:UN City Vienna.jpg|thumb|right|Jiji la UM pamoja na maao makuu ya IAEA huko Vienna, Austria]]
 
[[Image:Elbaradei.png|thumb|right|Mohamed Elbaradei Mkrugenzi wa IAEA]]
 
'''Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia''' ('''International Atomic Energy Agency (IAEA)''') ni mamlaka ya kujitawala ya kimataifa inayoshirikiana na [[Umoja wa Mataifa]] (UM). Ilianzishwa tar. [[29 Julai]] [[1957]] na nchi 81 wanachama wa UM.
 
Hata kama si moja kwa moja chini ya katiba ya UM inatoa taarifa zake kwa [[Mkutano Mkuu wa UM]] na [[Baraza la Usalama la UM]].
 
==Madhumuni==
Shabaha ya IAEA imekuwa tangu mwanzo matumizi ya nishati ya nyuklia yanayolingana na amani. Hapa imepewa madaraka ya kuangalia vituo vya kinyuklia katika nchi zote, kusaidia upanuzi wa teknolojia ya kinyuklia isiyo ya kijeshi na usalama wa matumizi ya nishati ya nyuklia. Shabaha muhimu ni pamoja na kuzuia uenezaji wa [[silaha za nyuklia]].
 
IAEA ni shirika la kimataifa linalopaswa kuangalia masharti ya [[mkataba wa kuzuia usambazaji wa silaha za nyuklia]] wa 1968.
 
==Muundo==
IAEA ina mikono mitatu:
*Mkutano Mkuu mwenye wawakilishi wa nchi wanachama 144 unakaa mara moja kila mwaka. Unakubali [[bajeti]] na kuamua juu ya maswali yanayowekwa mbele yake na halmashauri, na mkurugenzi mkuu au na wanachama wenyewe.
*Halmashauri ya Magavana inakaa mara tano kila mwaka na kufanya maazimio kuhusu mwelekeo wa kazi ya shirika; huwa na magavana 22 wanaochaguliwa na mkutano mkuu kwa muda wa miaka 2 halafu na magavana 13 wanaochaguliwa upya kila mwaka na halmashauri yenyewe.
 
*Ofisi Kuu inaongozwa na Mkurugenzi Mkuu pamoja makamu wake sita. Chini yao kuna wafanyakazi 2,200 pamoja na wanasayansi, mahandisi, watawala na wasaidizi. Mkurugenzi Mkuu tangu 1997 ni M[[misri]] [[Mohamed ElBaradei]].
 
Kazi inatekelezwa katika idara sita za utawala, sayansi ya nyuklia na matumizi yake, nishati nyuklia, usalama wa nyuklia, ushirikiano wa kiteknolojia na usimamizi wa vituo vya kinyuklia duniani.
 
Makao makuu yapo kwenye Jiji la UM huko [[Vienna]] ([[Austria]]). Ofisi za kanda zipo [[Toronto]] and [[Tokyo]], halafu kuna ofisi ndogo kwenye makao ya UM huko [[New York]] na [[Geneva]]. IAEA ina pia maabara ya uchunguzi katika Seibersdorf (Austria) na [[Monako]].
 
==Mafanikio na matatizo==
Udhaifu mmojawapo wa IAEA ni katiba ya kwanza inayodai kibali cha nchi wanachama kwa uchunguzi wa hali ya vituo vya nyuklia katika nchi hizi. Kwa njia hii nchi kadhaa ziliweza kuficha jitihadi zao za kuunda silaha za kinyuklia. Kwa sababu hiyo kuna mapatano mapya inayoruhusu wachunguzi wa IAEA kuingia katika maabara na taasisi ziote zinazoshughulikia mambo ya nyuklia wakati wowote. Ila tu haya mapatano mapya yalikuwbaliwa na nchi 73 pekee hadi 2006.
 
IAEA pamoja na mkurugenzi Mohamed ElBaradei ilipokea tuzo la Nobel la Amani maka 2005. Tuzo hili lilitolewa kwa sababu IAEA ilijitahidi kuzuia uvamizi wa Irak mwaka 2001.
 
Wataalamu wa UM walikuwa wametambua maabara ya kinyuklia nchini Irak yaliyofichwa kinyume na masharti ya mkataba wa kuzuia usambazaji wa silaha za nyuklia. Katika miaka kabla ya uvamizi wa Irak na Marekani IAEA ilifaulu kuchunguza maabara na ofisi nyingi hadi Irak haikuwa tena na utafiti wa kuunda silaha za nyuklia isipokuwa serikali ya Marekani haikuamini taarifa za IAEA na kushambulia Irak hata hivyo. Kamati ya Nobel iliamua ya kwamba IAEA ilijitahidi kuzuia matumizi ya kijeshi ya nishati ya nyuklia na kujenga matumizi salama ya nishati hii.
 
[[Category:Nishati]]
[[Category:Shirika za kimataifa]]
[[Category:Tuzo ya Nobel ya Amani]]
 
[[ar:الوكالة الدولية للطاقة الذرية]]
[[bn:আন্তর্জাতিক পরমাণু শক্তি সংস্থা]]
[[be-x-old:Міжнароднае агенцтва атамнай энэргіі]]
[[bg:Международна агенция за атомна енергия]]
[[ca:Agència Internacional de l'Energia Atòmica]]
[[cs:Mezinárodní agentura pro atomovou energii]]
[[cy:Yr Asiantaeth Ynni Atomig Ryngwladol]]
[[da:Det Internationale Atomenergiagentur]]
[[de:Internationale Atomenergieorganisation]]
[[et:Rahvusvaheline Aatomienergia Agentuur]]
[[en:International Atomic Energy Agency]]
[[es:Organismo Internacional de Energía Atómica]]
[[eo:Internacia Atomenergia Organizo]]
[[eu:Energia Atomikoaren Nazioarteko Agentzia]]
[[fa:آژانس بین‌المللی انرژی اتمی]]
[[fr:Agence internationale de l'énergie atomique]]
[[ko:국제원자력기구]]
[[hi:अंतर्राष्ट्रीय परमाणु ऊर्जा अधिकरण]]
[[id:Badan Tenaga Atom Internasional]]
[[is:Alþjóða kjarnorkumálastofnunin]]
[[it:Agenzia Internazionale per l'Energia Atomica]]
[[he:הסוכנות הבינלאומית לאנרגיה אטומית]]
[[kn:ಅಂತರರಾಷ್ಟ್ರೀಯ ಅಣುಶಕ್ತಿ ಪ್ರಾಧಿಕಾರ]]
[[kk:Атом қуаты халықаралық агенттігі]]
[[lb:International Atomenergie Agence]]
[[lt:Tarptautinė atominės energijos agentūra]]
[[hu:Nemzetközi Atomenergiai Ügynökség]]
[[mk:Меѓународна агенција за атомска енергија]]
[[ml:അന്താരാഷ്ട്ര ആണവോര്‍ജ്ജസമിതി]]
[[ms:Agensi Tenaga Atom Antarabangsa]]
[[my:IAEA]]
[[nl:Internationaal Atoomenergie Agentschap]]
[[ja:国際原子力機関]]
[[no:Det internasjonale atomenergibyrået]]
[[nn:Det internasjonale atomenergibyrået]]
[[pl:Międzynarodowa Agencja Energii Atomowej]]
[[pt:Agência Internacional de Energia Atómica]]
[[ru:Международное агентство по атомной энергии]]
[[sk:Medzinárodná agentúra pre atómovú energiu]]
[[sl:Mednarodna agencija za jedrsko energijo]]
[[sr:Међународна агенција за нуклеарну енергију]]
[[sh:IAEA]]
[[su:Badan Tanaga Atom Internasional]]
[[fi:Kansainvälinen atomienergiajärjestö]]
[[sv:IAEA]]
[[ta:பன்னாட்டு அணுசக்தி முகமையகம்]]
[[th:สำนักงานพลังงานปรมาณูระหว่างประเทศ]]
[[vi:Cơ quan Năng lượng Nguyên tử Quốc tế]]
[[tr:Uluslararası Atom Enerji Ajansı]]
[[uk:МАГАТЕ]]
[[bat-smg:Tarptautėnė atuomėnės energėjės agentūra]]
[[zh:国际原子能机构]]