Tofauti kati ya marekesbisho "Chipsi kuku"

9 bytes added ,  miaka 12 iliyopita
no edit summary
d (+jamii)
Karibu kwenye safu maridhawa na leo nalenga moja kwa moja kwa chakula mashuhuri chipsi kuku.
 
Utamaduni wa waswahili ambao hupatikana Afrika mashariki kwenye masuala ya maakuli, umemezwa na vibanda vya chipsi [[kuku]] katika mitaa mingi ya uswahilini.Neno maakuli linatokana na chimbuko la neno la kiarabu ikimaanisha mlo rasmi au maalum. Chakula cha chipsi kuku kimekuwa mashuhuri, ingawa vipo vingi kama mbatata za urojo, badia, kachori na chatne(Zanzibar mix au viazi vya karai). Biashara ya chipsi kuku imepanda chati, kwani inavutia wengi hasa kwenye michapuzo ya nguvu ambayo hukolezwa kwenye kilaji hicho cha chipsi kuku kama tomato sosi , chili sosi, rojo zito zito la embe mbichi au ukwaju na pilipili juu yake. Watafutaji ajira hamkani katika harakati za kuwaridhisha wateja wao, na wateja nao wake kwa waume humiminika kujipatia huduma hiyo, Alhamdulilah tumbo halilali na njaa.
 
Mandhari ya biashara hizi hutofautiana kutokana na vipato vya watafutaji ajira, kuna sehemu ambazo utastarehe na kiyoyozi juu yake, lakini sehemu nyengine kutokana na mazingira yake, fumba macho tu kama una njaa au waswahili wanasema ‘usimchungue kuku atakushinda kumla ‘. Lakini yote kenda , kumi mmeyaona [[mafuta]] yanayochomewa chipsi kuku ? Ikiwa kwenye karai au fraya. Haya mafuta yakipelekwa kwa mkemia mkuu sijui atatujibu nini. Faida ni kushiba lakini hasara hatuifahamu na nilazimani lazima tujiulize.
 
Tujali afya zetu kinga ni bora kuliko tiba.