Utengule/Usongwe : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 5:
 
==Historia==
Jina na mahali ni kihistoria; Utengule ilianzishwa na chifu Tovelamahamba [[Merere II]] wa [[Wasangu]] aliyepaswa kutoka [[Utengule Usangu]] baada ya kushambuliwa mara kwa mara na [[Wahehe]] chini ya [[Mkwawa]]. Alijenga Utengule mpya hapa Usafwa kwenye mtelemko wa mlima Mbeya mahali panapotazama bonde la [[mto Songwe]]. Utengule hii ya Merere II ilikuwa mji uliozungukwa na ukuta na sehemu za ukuta huu bado zinasimama kati ya mashamba na nyumba za kijiji. Merere akishirikiana na Wajerumani katika vita ya Wajerumani dhidi ya Wahehe na baada ya kifo cha Mkwawa Merere III alirudi Usangu alipojenga Utengule upya.
 
Kabla ya kuondoka Merere aliwahi kuwakaribisha wamisionari [[Wamoravian]] walioanzisha kituo cha nje ya mji wa Wasangu mwaka 1895 na kituo hiki cha Wamoravian kilikuwa kitovu kipya cha kijiji. Wamoravian walijenga kanisa, shule na karahana walipofundisha mafundi. Jengo la kanisa lipo hadi leo pamoja na chuo cha Biblia kinachosomesha wainjilisti wa [[Kanisa la Moravian kusini magharibi Tanzania]] (KMKMT). Askofu Mwafrika wa kwanza wa KMKMT [[Yohane Wawenza]] alikuwa mwenyeji wa Utengule.