Wilaya ya Nzega Vijijini : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
New page: '''Wilaya ya Nzega''' ni wilaya moja ya Mkoa wa Tabora nchini Tanzania. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 417,097 [http://www.tanzania.go....
 
No edit summary
Mstari 1:
'''Wilaya ya Nzega''' ni wilaya moja ya [[Mkoa wa Tabora]] nchini [[Tanzania]]. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 417,097 [http://www.tanzania.go.tz/census/census/districts/nzega.htm].
 
==Eneo la Nzega==
Imepakana na [[wilaya ya Kahama]] ([[mkoa wa Shinyanga|Shinyanga]]) upande wa kaskazini-magharibi, [[wilaya ya Tabora mjini]] upande wa kusini na [[wilaya ya Igunga]] upande wa mashariki.
 
Wilaya hii ina eneo la 9,226 [[km<sup>2</sup>]] na sehemu kubwa ni ardhi yenye rutba inayofaa kwa kilimo. Inapokea mvua milimita 9,000 kwa mwaka.
 
Sehemu kubwa ya eneo ni misitu inayozaa takriban 15,000 [[m<sup>3</sup>]] za ubao, makaa na kuni. Kuna mito inayozaa samaki na milambo 13. Mto muhimu ni mto Igombe unaovuka wilaya yote.
 
==Wakazi==
Wakazi wa wilaya ni hasa [[Wanyamwezi]] na [[Wasukuma]] walio wengi kuna pia [[Watutsi]] na [[Wanyiramba]]. Vikundi vingine ni [[Waarabu]] na [[Wachagga]] wanaotazamiwa kama wageni.
 
==Dini==
Dini kubwa ni Wakristo, Waislamu na wafuasi wa dini za jadi. Wakristo ni hasa Wakatoliki na Wapentekoste.
 
==Mawasiliano==
Barabara kuu inayoelekea [[Rwanda]] na [[Burundi]] inapita wilayani kuna njia za kwenda [[Shinyanga]], [[Mwanza]] na [[Tabora]]. Jumla ya barabara ni kilomita 1,137 lakini hakuna barabara za lami ni theluthi moja tu inayopitika mwaka wote.
 
[[Reli ya kati]] kutoka Dar es Salaam kupitia [[Tabora]] kwenda [[Shinyanga]] inapita wilayani pia.
 
Miji ya [[Nzega]] na [[Bukene]] ina simu na posta. Uenezaji wa simu za mkononi umesaidia mawasiliano nje ya miji hii.
 
==Elimu==
Kuna shule za msingi 196 na shule za sekondari 3 pamoja na chuo cha ualimu.
 
Vituo vya elimu ya watu wazima vilikuwa na wanafunzi 27,857. 65% za wakazi wote walikadiriwa kuwa wasomi. Kunauhaba wa madarasa, deski na nyumba za walimu.
==Afya==
Kuna hospitali mbili moja ni hospitali ya wilaya upande wa serikali na nyingine ni hospitali ya Ndala iliyoko chini ya kanisa katoliki. Kuna sahanati 4 za serikali na 1 ya kanisa katoliki. Kliniki 29 ziko chini ya serikali, 3 za watu binafsi na mbili za kanisa.
 
Huduma za afya hazitoshi ni chache kulingana na idadi ya watu. Tatizo kubwa ni hali mbaya ya chakula na wakina mama wengi kiasi wanakufa wakati wa kuzaa.
 
==Maji==
Takwimu ya 1993 ilionyesha ya kwamba chini ya nusu ya wakazi walikuwa na maji safi. Sehemu kubwa ni kutoka visima na wakati wa ukame maji huwa haba. Kuna hatari kubwa ya maji kuchafuliwa. Watu wengi hawana vyoo wala nafasi za kuacha takataka.
 
==Umeme==
Huduma za umeme zinapatikana Nzega mjini na kwenye makazi kadhaa yaliyopo kwenye barabara kuu Dar es Salaam – Rwanda - Burundi.
 
==Usalama==
Kuna vituo vya polisi, Force Unit (FFU), wanamigambo wa taifa na [[sungusungu]]. Kuna mahakama ya wilaya na mahakama ndogo 13 vijijini.
 
==Utawala na Siasa==
Kuna tarafa 4, kata 37, vijiji 134 na vijiji vidogo 969.
 
Wilaya ina majimbo mawili ya bunge ambayo ni Nzega na Bukene. Vyama vingi vilishindana kwenye uchaguzi. [[CCM]] ilipata kura nyingi ikashinda ikifuatwa na [[NCCR-Mageuzi]]
 
==Marejeo ya Nje==
*[http://www.redet.udsm.ac.tz/pilot_districts/nzega.php Nzega District Profile kwa Redet]
*[http://www.nzega.go.tz/Infrastructure.htm Nzega District Website]
 
 
{{tanzania-geo-stub}}