Tofauti kati ya marekesbisho "Shirikisho la Ujerumani"

24 bytes added ,  miaka 13 iliyopita
no edit summary
Nchi na maeneo ya kujitawala 38 zilijiunga ndani yake. Hizi zilikuwa nchi 34 zenye utaratibu wa kifalme (ufalme, utemi) na miji huru minne yenye katiba ya kijamhuri. Kila nchi ilijitawala na kujitegemea hata kimataifa.
 
Nchi mbili kubwa kati ya wanachama zilikuwa [[Dola la Austria]] na Ufalme wa [[Prussia]]. Zote mbili zilikuwa na maeneo makubwa ambayo yalihesabiwa kuwa nje ya eneo la shirikisho kwa sababu hazikuwahi kuwa sehemu za Dola Takatifu kabla ya 1806.
 
Shirikisho lilikuwa na nguvu wakati ambako Austria na Prussia zilishirikiana vizuri. Tangu [[1860]] na hasa tangu [[vita ya Schleswig ya 1864]] uhusiano ulikuwa mbaya na kusababisha [[vita ya Ujerumani ya 1866]] iliyomaliza shirikisho.
Tokeo la vita lilkuwa ya kwamba Austria ilibaki nje ya siasa ya Kijerumani; sehemu kubwa ya Ujerumani iliunganishwa katika Shirikisho la Ujerumani ya Kaskazini chini ya uongozi wa Prussia na madola ya Ujerumani kusini kama Bavaria yalibaki pekee.
 
Katika vita ya Ujerumani na Ufaransa nchi za Ujerumani kusini zilishikamana na Prussia. Tokeo lake likuwa kuundwa kwa [[Dola la Ujerumani]] tar. [[18 Januari]] [[1871]] mjini [[Versailles]] (Ufaransa).