Roberto Bellarmino : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created page with 'thumb Roberto Francesco Romolo Bellarmino alizaliwa Montepulciano (wilaya ya Siena nchini Italia) tarehe [[4 ...'
 
No edit summary
Mstari 5:
Alitangazwa na [[Papa Pius XI]] kuwa [[mwenye heri]] tarehe [[13 Mei]] [[1923]], [[mtakatifu]] tarehe [[29 Juni]] [[1930]] na [[mwalimu wa Kanisa]] tarehe [[17 Septemba]] [[1931]].
 
== Maisha ==
=== Utoto na ujana ===
Roberto alizaliwa katika familia kubwa, akiwa mtoto wa kiume wa tatu kati ya watano; wazazi wake walikuwa na asili ya kisharifu, lakini hali ya uchumi ilikuwa tofauti. Baba yake, Vincenzo Bellarmino alikuwa jaji, mama yake, Cinzia Cervini, alikuwa dada wa [[Papa Marcello II]].
 
Tangu utotoni alikuwa na afya mbovu na mwelekeo mkubwa kwa mambo ya [[dini]] kama mama yake. Baada ya kupata [[malezi]] nyumbani, alitumwa [[Padova]] kwa masomo.
 
Alipofikia umri wa miaka 18, akifuata [[wito]] wake wa [[upadri]], na kuvutiwa na mfano wa [[Ignas wa Loyola]], aliamua kujiunga na [[Shirika la Yesu]] alilolianzisha, na tarehe [[21 Septemba]] [[1560]] aliweka [[nadhiri]] zake za kwanza.
 
Bila ya kujivunia undugu wake na [[Papa]], alidumu kuwa na [[unyenyekevu]] na bidii.
 
Alisomea [[Roma]] tangu [[1560]] hadi [[1563]], halafu alianza kufundisha [[Firenze]] na [[Mondovì]], katika [[shule]] za shirika lake.
 
Mwaka [[1567]] alianza kusoma kwa mpango [[teolojia]] huko [[Padova]], lakini kutokana na sifa yake kama mhubiri, mwaka [[1569]] mkuu wa shirika, [[Fransisko Borja]], alimtuma [[Louvain]] (leo katika [[Ubelgiji]]), kwenye [[chuo kikuu]] maarufu cha mji huo. Ndipo alifahamu kwa karibu [[Uprotestanti]].
 
=== Ufundishaji ===
Baada ya kupata [[upadrisho]] huko [[Gand]] tarehe [[25 Machi]] [[1570]], alibaki Louvain miaka sita, hadi [[1576]] kama mwalimu wa teolojia na mhubiri, akizidi kupata wanafunzi na wasikilizaji kutoka kila upande.
 
Basi, [[Papa Gregori XIII]] alimuita Roma afundishe hoja dhidi ya [[uzushi]], kama alivyofanya hadi mwaka [[1587]]. Ni kwamba [[Mtaguso wa Trento]] ulikuwa umemalizika tangu muda mrefu, na Kanisa Katoliki lilikuwa na haja ya kujiimarisha kielimu na kiroho. Kazi ya Roberto iliingia moja kwa moja katika juhudi hizo za [[Urekebisho wa Kikatoliki]].
 
Kuanzia mwaka [[1588]], akiwa kiongozi wa kiroho wa [[Collegio Romano]], alishirikiana sana na [[Papa Sixtus V]], ingawa huyo hakumpenda sana yeye wala shirika lake. Kati ya vijana aliowalea, maarufu zaidi ni [[Alois Gonzaga]], ambaye alifariki mwaka [[1591]] kutokana na [[tauni]] aliyoambukizwa na mtu aliyemuokota barabarani. Baada ya kushughulikia [[kesi]] ya kumtangaza [[mwenye heri]], aliomba azikwe karibu naye, kama ilivyotokea baadaye.
Mwaka [[1592]] hadi [[1594]] alikuwa [[gombera]] wa seminari hiyo, halafu mwaka [[1595]] akawa mkuu wa shirika katika kanda ya [[Napoli]].
 
=== Ukardinali ===
 
Mwaka [[1597]] [[Papa Klementi VIII]] alimrudisha [[Roma]] kama mshauri katika masuala ya teolojia n.k.
 
Tarehe [[3 Machi]] [[1599]] Papa alimteua kuwa [[kardinali]] akieleza kwamba, ''Kanisa la Mungu halina mwingine sawa naye katika elimu''. Bellarmino alijaribu kwa kila njia kumfanya Papa abadili msimamo, lakini mwishoni alilazimika kukubali. Pamoja na hayo, hakubadili maisha yake magumu, na mapato yake aliyaelekeza karibu yote kwa maskini.
 
Kama kardinali aliongoza [[idara]] mbalimbali za Papa na kuwa [[Askofu mkuu]] wa [[dayosisi|jimbo]] la [[Capua]] ([[1602]]-[[1605]]).
 
Miaka ya mwisho alitunga [[katekisimu]] (kubwa na ndogo) iliyoenea sana hadi mwisho wa [[karne ya 19]].
== Maandishi ==
[[File:Roma-santignazio2.jpg|thumb|right|350px|TombaKaburi di Sanla Roberto Bellarmino nellandani ya [[ChiesaKanisa dila Sant'IgnazioMt. diIgnas wa Loyola inkwenye Campo Marzio]] ahuko Roma]]

[[Opera omnia]] zilizokusudia kukusanya maandishi yake yote Bellarmino zilitolewa [[Cologne]] ([[1617]]), [[Venezia]] ([[1721]]), [[Napoli]] ([[1856]]), [[Paris]] (1870).
 
Kati ya yale muhimu zaidi kuna haya yafuatayo:
Line 38 ⟶ 72:
 
== Viungo vya nje ==
*[http://www.catholic-hierarchyforum.orgcom/bishopsaints/bbella.html]saintr03.htm TaarifaMatukio muhimuya juumaisha yake katika Catholic forum web-site].
*[http://www.catholicism.org/de-laicis.html Kitabu De Laicis kuhusu serikali katika [[tafsiri]] ya [[Kiingereza]]]
[http://www.archive.org/stream/ajesuitcardinalr00ruleuoft/ajesuitcardinalr00ruleuoft_djvu.txt] Maisha yake.
*[http://www.cfpeople.org/Books/7Words/cfptoc.htm Kitabu Maneno Saba ya Yesu Msalabani]
*[http://www.archive.org/details/theeternalhappin00belluoft Kitabu Heri ya Milele ya Watakatifu]
*[http://www.archive.org/details/theartofdyingwel00belluoft Kitabu Ufundi wa Kufa Vema)]
*[http://goodcatholicbooks.org/pdf/bellarmine_art-of-dying-well.pdf Kitabu hichohicho katika PDF]
*[http://www.catholic-hierarchy.org/bishop/bbella.html]. Taarifa muhimu juu yake
*[http://www.archive.org/stream/ajesuitcardinalr00ruleuoft/ajesuitcardinalr00ruleuoft_djvu.txt] Maisha yake.
 
{{Walimu wa Kanisa}}
Line 46 ⟶ 86:
[[Jamii:Waliofariki 1621]]
[[Jamii:Wajesuiti]]
[[Jamii:MapadriMaaskofu Wakatoliki]]
[[Jamii:Makardinali]]
[[Jamii:Watakatifu wa Italia]]