Joseph Kony : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: pl:Joseph Kony
Replaced content with '((mbegu))'
Mstari 1:
((mbegu))
[[Image:JosephKony.jpg|frame|right|Joseph Kony]]
'''Joseph Kony''' (* mnamo [[1961]]) ni Mw[[uganda]] kutoka [[Acholi]] na mkuu wa jeshi la [[Lord's Resistance Army]] (LRA = ''Jeshi la Upinzani la Bwana'') ambali ni kikundi cha wanamigambo wa porini ambacho kimepigania vita dhidi ya serikali hadi [[2006]] kwa kuua watu wengi katika kaskazini ya Uganda na kuteka nyara watoto maelfu waliolazimishwa kuwa askari zake.
 
==Asili za Kony==
Kony alizaliwa katika kijiji cha Odek karibu na [[Gulu]] katika [[Acholi]]. Alibatizwa kuwa M[[katoliki]] hakumaliza shule.
 
Alimfuata shangazi yake [[Alice Lakwena]] katika vita ya [[Harakati ya Roho Mtakatifu]]. Baada ya kushindwa kwa Alice na mwisho wa jeshi lake Kony aliendelea kungoza kundi ndogo ya askari waliobaki pamoja.
 
==Sauti za mapepo==
Kony alidai kuwa alipokea sauti za mapepo pamoja na [[Roho Mtakatifu]] waliomwambia kuendelea na vita. Kony alidai ya kwamba shabaha ya vita ni kuanzisha utawala wa Mungu chini ya [[Amri Kumi]] za [[Biblia]].
 
==Mchanganyiko ya dini==
Wakimbizi waliofaulu kutoka katika makambi yake wamesema ya kwamba anatumia mchanganyiko wa dini mbalimbali:
* siku za [[Jumamosi]] alisali kwa namna ya kikristo na kutumia [[tasbihi]] kama Wakatoliki
* siku za [[Ijumaa]] alisali sala ya Al-Jummaa ya Waislamu
* alisheherekea [[Krismasi]]
* alifunga [[saumu]] wakati wa [[Ramadhani]]
* alikataza kula nyama ya [[nguruwe]]
* sadaka kwa mapepo zilitolewa kwa namna ya Kiacholi
* aliwaruhusu wanaume kuwa na wake wengi akawa mwenyewe na idadi kubwa ya wake
 
==Vita za Kony==
Kati ya 1987 - 1994 Kony aliendesha vita yake katika sehemu za Acholi katika kaskazini ya Uganda. Tangu 1994 alihamia [[Sudan]] ya Kusini kwa sababu ya mashambulio makali zaidi dhidi yake na jeshi al Uganda. Alijenga makambi kati Sudan -wengi wanasema alipata usaidizi wa serikali ya Sudan iliyochukizwa na msaada wa [[Kampala]] kwa ajili ya [[SPLA]]- na kushambulia ndani ya Uganda. Wakati ule askari zake walianza kulipiza kisasi kwa Waacholi waliodhaniwa kuwa walishirikiana na serikali kwa kuwaua au kukata mikono, masikio, miguu au midomo ya watu.
 
Tangu [[1994]] aliamuru pia kutekwa nyara kwa watoto na vijana waliolazimishwa kutembea hadi [[Sudan]]; wavulana waliingizwa katika jeshi lake na wasichana walichukuliwa kama "wake" wa askari zake; Kony anasemekana alipenda kuchagua kati ya mabinti hawa.
 
Mwaka [[2002]] jeshi la Uganda ilipatana na Sudan ikapata kibali cha kushambulia makambi ya Kony ndani ya Sudan. Jibu la Kony ilikuwa kurudi Uganda na kuwaua watu wengi zaidi kuliko awali lakini jeshi la Uganda iliongeza pia askari zake.
 
==Mashtaka mbele ya [[Mahakama Kuu ya Kimataifa]]==
[[2003]] Kony pamoja na viongozi wenzake walishtakiwa mbele ya [[Mahakama Kuu ya Kimataifa]] kwa hatia za
* jinai dhidi ya ubinadamu na mauaji
* jinai ya kuteka watumwa
* jinai ya ubakaji
* matendo ya kinyama ya kuumiza watu (kukata viungo vya mwili)
* kuumiza watu raia (wasio wanajeshi) kwa kusudi
* kuwalazimisha watoto wadogo kuwa wanajeshi
 
Mwaka 2005 LRA ililazimishwa kuhamisha kambi lake ndani ya [[Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo]] lakini iliendelea kushambulia sehme zu Uganda ya Kaskazini.
 
==Majadiliano ya 2006 juu ya amani==
Mwaka 2006 Kony alimruhusu makamu wake [[Vincent Otti]] kuanzisha majadiliano na serikali ya [[Yoweri Museveni]]. Majadiliano yalifanyika mjini [[Juba]] katika Sudan.
 
Kony na viongozi wenzake waliahidi ya kwamba watamaliza vita na kuwaruhusu askari warudi kwao wasipokamatwa na kupelekwa mahakamani.
Agosti 2006 LRA ilitangaza kusimamisha vita.
 
Kati Septemba 2006 vikosi ya LRA vilianza kurudi Uganda na kukutana na wanajeshi wa serikali waliowaongoza kuelekea makambi.
 
 
== Viungo vya Nje ==
* [http://www.acholiteck.com/ About The Acholi People]
* [http://www.acholinet.com/ Acholi Community Web Portal]
* [http://www.africanfront.com/page600.php I want peace, but Museveni is the problem, says Kony ], transcript of Joseph Kony's call in to a political talk show on the Mega FM radio station broadcasting from Gulu on [[28 December]] [[2002]]
* [http://www.newvision.co.ug/D/8/12/443579 Kony's eldest son killed], [[New Vision]], [[8 July]] [[2005]]
* [http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/4320858.stm Profile: Ugandan rebel Joseph Kony], BBC News, last updated [[7 October]] [[2005]]
* J. Carter Johnson, [http://www.christianitytoday.com/ct/2006/001/18.30.html?lid=ct_deliver_us_title&1pos=main Deliver Us from Kony], [[Christianity Today]], January 2006
* [http://www.mg.co.za/articlePage.aspx?articleid=263835&area=/insight/insight__africa/ Portrait of Uganda's rebel prophet, painted by wives], [[Mail & Guardian]], [[10 February]] [[2006]]
* Sam Farmar, [http://news.bbc.co.uk/2/hi/programmes/newsnight/5124762.stm Uganda rebel leader breaks silence] (interview with downloadable audio in MP3 format), BBC [[Newsnight]], [[28 June]] [[2006]]
* Ruud Elmendorp, [http://www.videoreporter.nl Joseph Kony gives press conference] (video report from Joseph Kony in his outpost in the Congo), Ruud Elmendorp, [[2 August]] [[2006]]
* [http://www.rocketboom.com/vlog/archives/2006/08/rb_06_aug_16.html Ruud Elmendorp's video interview with Joseph Kony] on [[Rocketboom]] [[16 August]] [[2006]]
* Ochola John, [http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/5129350.stm LRA victim: 'I cannot forget and forgive'], BBC, [[29 June]] [[2006]]
 
 
[[Category:Watu wa Uganda]]
[[Category:Vita vya msituni Afrika]]
 
[[de:Joseph Kony]]
[[en:Joseph Kony]]
[[es:Joseph Kony]]
[[fi:Joseph Kony]]
[[fr:Joseph Kony]]
[[he:ג'וזף קוני]]
[[id:Joseph Kony]]
[[it:Joseph Kony]]
[[ja:ジョゼフ・コニー]]
[[nl:Joseph Kony]]
[[no:Joseph Kony]]
[[pl:Joseph Kony]]
[[pt:Joseph Kony]]
[[ru:Кони, Джозеф]]
[[sv:Joseph Kony]]
[[tr:Joseph Kony]]