Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Mr Accountable (majadiliano) 11:35, 24 Novemba 2009 (UTC)Reply

Makala hariri

Ndugu Chamaroa, salam! Umeandika makala nyiingi, lakini zote utumbo mtupu. Yaani, ulichojua wewe ni kuanzisha na kuweka alama ya KWC na MBEGU tu, basi. Hii siyo mwenendo mzuri na si muda sana kutoka sasa makala zako zote zitafutwa! Na ukiendelea na mwenendo huu, basi tegemea kufutwa makala zako kila uanzishapo. Pole sana, ndugu. USHAURI: Unaombwa na kushauriwa upitie ukurasa wa Wikipedia:Mwongozo. Huo utakusaidia namna ya kuandika na kufuata mwongozo mzima wa uandikaji wa Wikipedia ya Kiswahili! Tuendeleee!!!--  MwanaharakatiLonga 06:41, 19 Desemba 2009 (UTC)Reply

Ndugu, naona bado unaendelea kuandika makala bila maneno yoyote yale. Tena kibaya zaidi bado unaandika makala tena bila lolote zaidi ya kigezo cha MBEGU. Kaka, hii si taratibu nzuri. Maadamu nilikutaarifu na hukuelekea kuelewa au hata kuuliza tena, basi kisu kinapita kwa makala yale yote uliyoanzisha!--  MwanaharakatiLonga 06:39, 21 Desemba 2009 (UTC)Reply

makala zihitajizo habari hariri

Ndugu Chamaroa, salaam! Wakati wa shindano, makala nyingi zimeanzishwa bila kuwekewa yaliyomo hata kidogo, nasi wanawikipedia hatukuwa na nafasi ya kurekebisha sana. Kwa hiyo sasa, naomba tusaidiane kusawazisha hizo makala. Kwa mfano, ungeweza kuanza kwa kuangalia orodha ya makala bila jamii. Bila shaka utagundua kadhaa ambazo ni duni, labda yenye maneno mawili matatu tu. Ndivyo nilivyogundua k.m. na makala ya Henri Fayol, mhandisi Mfaransa wa karne ya 19. Sasa ukiangalia mabadiliko niliyoyaingiza utapata mambo ya msingi ya wikipedia. K.m. naingiza kigezo cha {{DEFAULTSORT}} kwa ajili ya orodha ya makala katika jamii ifuate alfabeti vizuri. Tena naingiza jamii za miaka ya kuzaliwa (k.m. [[Jamii:Waliozaliwa 1841]]) na ya kufariki (k.m. [[Jamii:Waliofariki 1925]]). Pia, ikiwa ni makala fupi bila maelezo mengi, naingiza kigezo cha {{mbegu-mtu}} (yaani kama ni mtu). Hatimaye, naingiza kiungo kwa wikipedia ya Kiingereza (k.m. [[en:Henri Fayol]]) ambapo naweza kupata code kwa picha ya mtu (k.m. [[Image:Fonds henri fayol.jpg|thumb|right|Henri Fayol]]) pamoja na habari nyingine. Nitashukuru kwa msaada wako katika kuboresha makala mpya zilizoachwa duni. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 12:05, 2 Februari 2010 (UTC)Reply

Joseph Kony hariri

Bwana Chamaroa salamu! Nimeona na kufurahia jinsi ulivyopanusha makala kuhusu Joseph Kony ukafanya kazi kubwa. Ila tu nina neno naomba uangalie upya kwa sababu hizi a) nakala ilikuwepo tayari na wewe ulifuta maandishi yote yaliyokuwepo awali; hii hatutakiwi kufanya bila kuonya kwanza kwenye ukurasa ya majadiliano (tukiona makosa mazito au kama makala ilikuwa fupi mno ya kutoridhisha) b) ni saswa kabisa kupanusha makala, kuongeza habari na kusahihisha makosa lakini kufuta bila taarifa ya awali tusifanye. Kwanza kwa sababu ni verma kuheshimu kazi iliyotangulia (hata kama ilikuwa ya makosa) pili kuepukana na ugomvi kati ya waandishi. c) uliongeza habari nyingi lakini muundo wa awali ulipendeza zaidi (picha, vichwa vidogo vya kumsaidia msomaji)

Kwa hiyo naomba uangalie upya. Ushauri wangu:

  • rudi katika hali ya uhariri, kopi yote na kuihifadhi katika ukurasa wa Word (au programu unayotumia)
  • fungua "historia" ya makala na ingia katika hali ya makala kabla ya hujaandika.
  • humo ongeza habari zako za ziada chini ya vichwa husika au kwa kuunda vichwa vipya.
  • halafu hafadhi yote kama umbo mpya wa nakala.

Ukihitaji msaada niko tayari kukusaidia. Katika utaratibu wa wikipedia ningefanya revert tu lakini hii inamaanisha kufuta kazi yako yote na sitaki kukukatisha moyo kwa hiyo naomba tuwasiliane jinsi gani kuunganisha umbo la awali na umbo lako. Kipala (majadiliano) 12:15, 26 Mei 2010 (UTC)Reply