Muddyb

Joined 18 Agosti 2007
sahihisho dogo tu.
(sahihisho dogo tu.)
{{Msanii muziki 2 <!-- See Wikipedia:WikiProject_Musicians -->
| Jina = Muddyb Blast Producer
| Img = Muddyb-2010.jpgJPG
| Img_capt = Muddyb Blast nikiwa kwenye pozi!
| Img_size =
| Ala zinazojulikana =
}}
Ninaitwa Mohammed. Humu hujiita "'''{{BASEPAGENAME}}'''". Ninaishi [[Dar es Salaam]], [[Tanzania]]. Hapa ninasimama kama mkabidhi na mrasimu wa [[kamusi elezo]] hii ya [[Kiswahili]]. Ukiwa una uswali lolote, basi uliza nami nitakujibu! Mimi ni mpenzi sana wa muziki na filamu. Hivyo, makala nyingi ninazoandika zinahusu masuala ya muziki na filamu!
'''Mohammed George''' au '''Muddyb Blast Producer''' (nimezaliwa tar. [[25 Aprili]], [[1983]]) ni mwanaharakati wa kweli wa Wikipedia, niliyejitolea kuendeleza kamusi elezo huru ya Kiswahili kwa muda usiojulikana lini nitaacha kuchangia makala katika kamusi elezo hii ya Kiswahili. Ni mda sasa toka nijiunge na wikipedia ya Kiswahili, na nimekuwa nikifanya doria za hapa na pale katika wiki hii ya Kiswahili.
==Wasifu==
===Maisha ya Awali===
Nimezaliwa na kukulia [[Dar es Salaam]], [[Tanzania]]. Baba yangu ni mtu wa [[Tanga]] (kabila lake [[Wazigua|Mzigua]]), na mama yangu mtu wa Kilwa, Lindi (Myao). Nimesoma na kumalizia elimu yangu yote [[Dar es Salaam]] kwa wajanja [[Tanzania]].
 
Vilevile mimi ni mmoja wa wapenzi wa muziki na filamu duniani hakuna, ukibisha yauri yako lakini mie ndiyo nasonga mbele. Kwa sasa niko nafanya makamuzi yangu katika kampuni fulani hivi ya hapa Mjini Dar es Salaam, na vilevile ninasaidi hapa katika Wikipedia hii ya Kiswahili.
 
Pia, napenda kuwakaribisha mavijana wenzangu, mababu na mabibi wakiwemo na watoto wenye ufahamu wa kutumia zana za kisasa yaani Kompyuta, tushirikiane kuendeleza kamusi ya Waswahili!
 
==Maisha ya Kidunia==
Makuzi yangu yote yalikuwa jijini Dar es Salaam Tanzania, na sijawahi kwenda mkoa wowote ule wa nchini kwetu. Ila najivunia kwa kuzaliwa katika jiji lenye kila kitu, bahari, majumba ya sanaa, starehe mbalimbali, wanamuziki wenye akili kibawa wapo huku, serikali halisi ipo huku, watoto wazuri (wachumba) na mambo mengine mengi tu yapo huku.
 
Hapo awali , nilikuwa na jina la utani lililojulikana kama Muddy Baby, kwasababu nilikuwa bwana mdogo niliokuwa hatari katika maswala ya kuruka sarakasi (jamani niliwatingisha!!) eeh usipime.. Kadri miaka inavyozidi kwenda majina yanaongezeka, baadaye wakaniita Muddyb kiwakilisho cha neno baby wakalikata ikawa b yaani Muddyb ndio hadi sasa natumia jina hilo.
 
Blast lilikuja baadaye baada ya kuwa napenda sana nyimbo za [[Hip hop]] kupindukia, na vile nikiwa naziimba ndio masela wangu wakaniita Blast Mnyamwezi (Mnyamwezi maanake mtu anayependa hip hop ya kweli) na nikawa natengeneza ala za muziki wa hip hop bila ya Bongo Flava!! Basi ebwanaee toka kipindi hicho ikawa noma mtu wangu hadi leo hii.
 
==Maisha ya katika wikipedia na michango yake==
Muddyb nilijiunga rasmi na Wikipedia mnamo tar. [[18 Agosti]] mwaka 2007, nimenuiya kuendeleza mradi huu wa wiki na nitaendelea mpaka sijui lini yaani. Toka kipindi hicho nilichoingia hapa nimetoa michango yangu kadhaa. Zaidi na zaidi, nachangia makala za kuhusiana na [[filamu]] na [[muziki]]! Na mara chache ushiriki kwenye makala za miji na watu mashuhuri na wenye historia maridhawa duniani. Hebu soma hapo chini upate kujua nimehariri mara ngapi na kuendelea:
 
*Hadi sasa nimehariri mara '''11,247+'''
*Pia unaweza kuangalia michango yangu endelevu kwa kukong'oli hapo chini:
 
Angalia michango yangu endelevu:
 
*[[Maalum:Michango/Muddyb_Blast_Producer|Michango Yangu]]
 
Ukiwa unaswali lolote kuhusiana na wikipedia hii nitakueleza kama hilo swali nalijua namna ya kulijibu. Jamani karibuni.
 
==Masanduku vya Mtumiaji==
{{User sw}}{{User en-2}}