Baraza la Kiswahili la Taifa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
iw
majukumu ya BAKITA
Mstari 3:
 
Pamoja na Chama cha Kiswahili cha Taifa ([[CHAKITA]]) cha Kenya na wawakilishi kutoka Uganda BAKITA imeunda Baraza la Kiswahili la Afrika Mashariki ([[BAKAMA]]).
==Majukumu ya BAKITA==
# Kukuza maendeleo ya matumizi ya lugha ya Kiswahili mahali pote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
#Kushirikiana na vyombo vingine katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambavyo vinahusika na uendelezaji wa lugha ya Kiswahili na kuratibu kazi zao.
#Kuhimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli za Serikali na kwa shughuli za umma.
#Kuhimiza matumizi fasaha ya lugha ya Kiswahili na kuzuia upotoshaji wake.
#Kushirikiana na mamlaka yanayohusika katika kuanzisha tafsiri sanifu ya istilahi za Kiswahili.
#Kwa kushirikiana na vikundi vyovyote vya kimataifa, taasisi, au kundi la watu, na watu binafsi kufuatilia, kushauri na kuratibu shughuli zinazolenga kukuza Kiswahili.
#Kuchunguza vitabu vya au maandishi yaliyoandikwa na kufasiriwa katika Kiswahili na kuhakikisha kwamba lugha iliyotumika ni sanifu na inakubaliwa na Baraza.
#Kutoa huduma za tafsiri kwa mashirika, idara, wizara, Balozi na watu binafsi
#Kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu ya Taifa kuthibitisha vitabu vya kiada vya Kiswahili kabla ya kuchapishwa, kwa ajili ya Taasisi za Elimu.
#Kuratibu na kutoa huduma za ukalimani kwenye mikutano ya kitaifa na kimataifa ndani na nje ya nchi.
 
==Viungo vya Nje==