ANC : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
CGN2010 (majadiliano | michango)
No edit summary
Mstari 3:
 
== Kuanzishwa kwa ANC ==
ANC ilianzishwa mjini [[Bloemfontein]] tar. [[8 Januari]] [[1912]] kwa jina la "South African Native National Congress". Jina la "Congress" lilichaguliwa kufuatana na mfano wa chama cha Kinhindi cha "[[Indian National CiongressCongress]]" ilikuwa chama cha kwanza katika koloni za Uingereza kilichodai mabadiliko ya ukoloni kwa njia ya kisiasa. Madai ya ANC yalikuwa hasa haki kwa ajili ya wakazi asilia katika nchi mpya ya [[Umoja wa Afrika Kusini]]. Mwaka 1924 jina likabadilishwa kuwa "African National Congress".
 
Chama kilidai haki sawa kwa wakazi wote bila kujali rangi yao. Mwendo huu uliunganisha Waafrika kutoka pande mbalimbali kama vile wasomi, machifu, viongozi wa kanisa na wengine. Wanawake walikubaliwa tangu 1931 na 1943 wakapewa haki zote za uanachama.