Maradhi ya zinaa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
kusafinisha sentensi ya kwanza
d Bot: Simplifying links ([link|linktext] → [link]text)
Mstari 31:
Magonjwa ya zinaa huambukizwa na wakala wa magonjwa – [[bakteria]] wadogowadogo, [[virusi]], [[parasites]], [[fungi]] na [[protozoa]] wakaao katika sehemu vuguvugu na zenye unyevunyevu katika mwili kama vile [[sehemu za siri]], [[mdomoni]] na [[kooni]]. Magonjwa mengi ya zinaa husambaa wakati wa [[kujamiiana]] (katika [[uke]] au mkunduni), lakini aina nyingine za kukutana kimapenzi kama kwa kutumia midomo (''oral sex'') zinaweza kusambaza magonjwa.
 
Magonjwa mengine ya zinaa yanaweza kusambazwa kwa njia nyingine zaidi ya [[kujamiiana]]. Magonjwa fulani ya zinaa yanayosababishwa na [[virusi]] kama [[ukimwi|UKIMWI]] yanaweza kuambukizwa kwa kukutana na [[damu]] iliyoathirika. Kwa mfano, magonjwa yanayosababishwa na virusi yanaweza kusafiri miongoni mwa watu wanaochangia sindano zilizo na maambukizi, na mtu anaweza kupata maambukizi kwa kupokea dawa iliyoambukizwa. Baadhi ya magonjwa ya zinaa huambukiza kwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto. Maambukizi yanaweza kutokea kabla ya kuzaliwa, wakati vijidudu vikifanikiwa kupita katika [[kondo la uzazi]] (''placenta'', ogani katika [[mji wa mimba]] wa [[mwanamke mjamzito]] ambayo huunganisha mfumo wa damu ya mama na wa mtoto) na kuingia katika mkondo wa damu wa mtoto. Maambukizi pia huweza kutokea wakati wa kujifungua, wakati mtoto anapopita katika njia ya uzazi au baada kujifungua, wakati mtoto anapotumia [[maziwa]] yaliambukizwa.
 
Magonjwa ya zinaa hayawezi kuambukizwa kwa kupeana mikono au kugusana, au kugusa nguo au katika viti vya chooni.
Mstari 106:
=== UKIMWI ===
 
[[ukimwi|UKIMWI]], Ukosefu wa Kinga Mwilini, ni matokea ya maambukizi ya [[virusi vya Ukimwi]] (VVU) - ''Human immunodeficiency virus'' (HIV). [[ukimwi|UKIMWI]] ni ugonjwa wa zinaa hatari na usitibika ambao hushambulia [[mfumo wa kinga ya mwili]] na kumwacha mgonjwa akiwa hana hata uwezo wa kujikinga dhidi ya maambukizi madogo. Maambukizi ya VVU haimaanishi kuwa mtu ana [[ukimwi|UKIMWI]]. Baadhi ya watu na maambukizi ya VVU na wasionyeshe hali ya kuumwa ile inayotambulika kama UKIMWI kwa miaka kumi au zaidi. Watabibu hutumia neno [[ukimwi|UKIMWI]] pale mtu anapokuwa katika hatua za mwisho, zinazotishia uhai za maambukizi ya VVU.
 
UKIMWI uligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka [[1981]] miongoni mwa wanaume waliokuwa wanaingiliana (mashoga) na miongoni mwa watu waliokuwa wanajidunga sindano katika jiji la [[New York]] na [[California]]. Baadaye maambukizi mengine yaligundulika pia kusini mwa [[jangwa la Sahara]] barani [[Afrika]]. Kwa haraka UKIMWI ukawa [[ugonjwa wa mlipuko]] duniani kote ukiathiri karibia kila nchi. Mpaka mwaka [[2002]], ilikadiriwa kuwa watu wazima wapato milioni 38.6 na watoto milioni 3.2 duania kote wanaishi na [[VVU]] au [[ukimwi|UKIMWI]]. Shirika la Afya Ulimwenguni, [[WHO]], limekadiria kuwa kutoka mwaka [[1981]] mpaka mwisho wa mwaka [[2002]] watu karibia milioni 20 walikuwa wamekufa kutokana na [[ukimwi|UKIMWI]]. Kiasi cha hao milioni 4.5 walikuwa ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 15.
 
Wakati [[VVU]] wanaweza kuenezwa kwa njia nyingine, kujamiiana ndiyo njia hasa ya maambukizi ya virusi hivi. Wanawake ambao wameathirika na virusi vya [[ukimwi|UKIMWI]] wanaweza kumwambukiza mtoto wakati wa ujauzito, kujifungua, au mara kadhaa wakati wa kuwanyonyesha. Njia mbadala ya kupunguza makali ya VVU ni pamoja na kutumia madawa yanayozuia kuzaliana kwa VVU (''protease inhibitors''), ambayo husaidia kwa kiasi kikubwa kurefu maisha.
 
Pamoja na kuenea kwa elimu juu ya ugonjwa huu, CDC wamekadiria kuna maambukizi mapya 40,000 kila mwaka [[Marekani]] na kuwa kwa ujumla kati ya [[Waamerika]] 800,000 hadi 900,000 wameambukizwa [[VVU]].
Mstari 142:
Hata hivyo kuanzia miaka ya [[1950]], huko [[Marekani]] [[kisonono]] kilianza kuenea kutokana na kuongezeka kwa tamaa za ngono. Vijidudu vya ugonjwa viliunda ukinzani dhidi ya [[penicillin]], na mpaka miaka ya [[1970]] na [[1980]] ugonjwa ulifikia hatua ya kuwa ugonjwa wa mlipuko kwa vijana na watu wa [[umri wa kati]].
 
Kuingia kwa [[VVU]] katika jamii ya [[binadamu]] kumepelekea janga la kimataifa la [[ukimwi|UKIMWI]] ambalo lilianza katika miaka ya [[1980]] na kuendelea hadi leo hii.
 
Majanga ya magonjwa ya zinaa yanaendelea, hata pamoja na [[utumiaji wa kondomu]] ambao umeongezeka tangu kuanza kwa [[ukimwi|UKIMWI]]. Maafisa wa afya wanaamini kuna mambo mengi yanayowezekana kuwa yanachangia kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Miongoni mwao ni mienendo ya [[tabia hatarishi]]. Katika miongo kadhaa iliyopita, umri ambao watu hufanya [[ngono]] kwa mara ya kwanza umepungua, wakati wastani wa wenzi wa kimapenzi ambao mtu hufanya nao ngono katika kipindi cha maisha yake umeongezeka. Kwa pamoja mienendo hii huongeza hatari ya kupata magonjwa ya zinaa.
 
== Angalia Pia ==
 
* [[ukimwi|UKIMWI]]
* [[Kisonono]]
* [[Kaswende]]