Maji kujaa na kupwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
nyongeza kidogo
viungo
Mstari 1:
[[File:Bay of Fundy.jpg|thumb|300px|Bandari ya Alma katika Kanada kwenye pwani la Atlantiki wakati wa maji kujaa na kupwa.]]
[[Picha:England-Saint-Michaels-Mount-1900-1.jpg|thumb|200px|Kisiwa cha Saint Michaels Mount nchini Uingereza hufikiwa kwa miguu kwenye nchi kavu wakati wa maji kupwa]]
'''Maji kujaa na kupwa''' ni mabadiliko ya uwiano wa [[bahari]] unaopanda na kushuka kila siku. "Maji kujaa" ni hali ya juu na "maji kupwa" ni hali ya chini ya maji ya bahari. Tofauti kati ya hali hizi inaweza kufikia hadi mita kadhaa.
 
Mabadiliko ya maji kujaa na kupwa hutokea mara mbili kila siku yaani kila mahali huwa na maji kujaa mara mbili na maji kupwa mara mbili kila siku.
 
==Kanda la kujaa na kupwa==
Kwenye pwani ambako mtelemko wa nchi si mkali kuna kanda ya eneo linalobadilika kila siku kuwa nchi kavu kwa masaa kadhaa halkafuhalafu tena bahari. Karibu na [[Mombasa]] kuna kanda la pwani ambako bahari inarudi kila siku kwa upana wa kilomita mbili na wakati wa maji kupwa inawezekana kutembea kwa kilomita hizi mbili ambako baada ya masaa kadhaa bahari itarudi.

Katika nchi nyingine kanda hili linaweza kufikia hadi ya upana wa kilomita 40 kwa mfano kwenye pwani la [[Bahari ya Kaskazini]] upande wa [[Ujerumani]] na [[Uholanzi]].
 
Kanda hili ni muhimu kwa ajili ya ekolojia ya bahari maana vidudu vingi ambavyo ni lishe ya samaki na ndege wanaishi na kuzaa hapa.