Koreshi Mkuu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza simple:Cyrus the Great
nyongeza
Mstari 7:
 
==Familia==
Nasaba ya Akhameni ilianzishwa na mwajemi Akhameni aliyekuwa mtawala wa eneo dogo la Uajemi kusini magharibi ingawa wakati ule hapakuwa na "Uajemi" bado; sehemu kubwa ya nchi ilitawaliwa na [[Wamedi]] waliokuwa kabila ya Uajemi ya magharibi. Mwanawe Teispes alipanusha eneo hili hadi kushika [[Pars]] ambayo ni kiini cha Uajemi mwenyewe. Mwanawe [[Koreishi I]] akafuatwa na [[Kambisi I]] aliyekuwa baba wa Koreishi II anayejulikana kama Koreishi Mkuu.
Nasaba ya Akhameni ilianzishwa na mwajemi Akhameni aliye
 
Hadi hapa watawala hao walisimamia maeneo madogo wakipaswa kutii mabwana wao hasa Wamedi. Koreishi Mkuu aliasi dhidi ya Bwana wake na kutwaa utawala wa milki ya Wamedi akaendelea kutwaa nchi jirani.
 
==Kuzaliwa na maisha==
Mwandishi Mgiriki [[Herodoti]] anasimulia ya kwamba wazazi wa Koreishi walikuwa [[Kambisi]] I na Mandane, binti wa mfalme Astyages wa Media. Baadaye mfalme Astyages alikuwa na ndoto iliyomwambia ya kwamba mjukuu atakuwa hatari kwake. Kwa hiyo alimtuma [[jenerali]] yake Harpagus kumwua mtoto wa binti yake na huyu mtoto alikuwa Koreishi. Lakini jenerali Harpagus hakutaka kumwaga damu ya kifalme akamtwaa mtoto na kumpa mchungaji mmoja wa kondoo aliyemzaa wakati huohuo mtoto aliyekufa mara moja. Mchungaji alimpokea Koreishi akamlea na Hapagus alimwonyesha mfalme maiti ya mtoto mchanga.
 
Koreishi alipofikia umri wa miaka 10 alitambuliwa kama mtoto wa kifalme. Astyages aliamua kumhurumia sasa akamtuma kwa wazazi wake. Lakini jenerali Harpagus aliadhibiwa vikali kwa sababu alimwalika kwa chakula katika ikulu yake na kwa siri aliamuru kumwua mtoto wake Harpagus, kumpika, kumkatakata na kumweka mezani ili Harpagus ale. Hivyo jenerali alikuwa adui wa mfalme.
Mwaka [[559 KK]] Koreishi alimfuata babake kama mtawala wa kieneo. Harpagus aliwasiliana naye na kumchochea hadi Koreishi aliasi dhidi ya mfalme Astyages mwaka [[553 KK]]. Baada ya vita ya miaka 3 mfalme alishindwa [[550 KK]], Koreishi akawa mfalme wa Media na Uajemi.
 
Koreishi alimwoa mke kwa jina Kassandane aliyetoka katika kabila lake. Walizaa watoto wanne kati yao [[Kambisi II]] aliyemfuata baba baadaye na binti Atossa aliyekuwa mama wa mjukuu wake [[Xerxes I]]. Kassandane alipokufa mapema Koreishi alionyesha huzuni kuwa sana. Kufuatana na taarifa kadhaa alimwoa baadaye mke kutoka kwa Wamedi.
 
==Mfalme wa Uajemi na Media==
Baada ya ushindi wake Koreishi Mkuu aliendelea kutumia [[Ekbatana]] mji mkuu wa Wamedi kama makao makuu wakati wa miezi ya joto. Kwa majira ya baridi alijenga mji mkuu mpya Pasargadae katika Pars. Akitumia cheo cha "Mfalme wa Uajemi na Medi" akaenddlea kudai utii kutoka milki zote zilizowahi kuwa chini ya usimamizi ya Medi.
 
==Upanuzi wa milki==
Hivyo akafanya vita dhidi ya watawala wengi wasiotaka kumkubali; alianza katika Anatolia ya mashariki alipovamia Urartu, akaendelea hadi miji ya Wagiriki katika Anatolia ya magharibi. Hadi mwaka [[540 KK]] aliwashinda na kuwaweka chini ya mamlaka yake.
 
Mwaka 539 alipiga vita dhidi ya milki ya Babeli na 23 Oktoba [[539 KK]] Koreishi aliingia Babeli kama mshindi akapokea cheo cha mfalme wa Babeli.
 
Mwaka uliofuata alimpa mwanawe Kambisi cheo cha mfalme wa Babeli na Koreishi mwenyewe alijiita "Mfalme wa wafalme".