Kanieneo angahewa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza simple:Atmospheric pressure
No edit summary
Mstari 2:
'''Kanieneo angahewa''' ni nguvu inayosukuma dhidi ya uso wa dunia na kila kitu au kiumbe kutokana uzito wa [[hewa]] iliyoko katika [[angahewa]] ya dunia juu yake.
 
==Uzito wa hewa==
Juu ya kila mahali duniani kuna uzito wa nguzo ya hewa yenye urefu wa takriban kilomita 500 hadi mwisho wa angahewa. Uzito huu ni mkubwa kwenye pwani la bahari ambako ganda la hewa juu ya mahali ni nene. Lakini uzito huu na hivyo kanieneo ni mdogo zaidi juu ya milima mirefu ambako umbali hadi mwisho wa angahewa ni mdogo zaidi. Kwa wastani uzito wa nguzo ya hewa juu ya [[mita ya mraba]] moja kwenye [[uwiano wa bahari]] ni [[tani]] 10 lakini kipimo hiki kinaonyesha mabadiliko kutokana na mabadiliko ya kanieneo angahewa mahali hapa.