Mwezi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Minor fix using AWB
Mstari 1:
[[Picha:Earth-Moon System.jpg|right|thumb|200px|[[Chombo cha angani Galileo]] ilipiga picha hii ya Ardhi na mwezi]]
[[Picha:NASA-Apollo8-Dec24-Earthrise.jpg|right|thumb|200px|Picha maarufu sana ya dunia yetu iliyopigwa na [[mwanaanga]] Mmarekani [[Bill Anders]] wakati wa ujumbe wa [[Apollo 8]] tarehe Disemba 24, Desemba 1968. Apollo 8 ilikuwa mara ya kwanza chombo cha angani cha kubebea watu kushikwa na graviti ya mwezi na kuzunguka mwezi kwa ajili ya [[graviti]] hiyo. ]]
 
 
Mstari 8:
Sayari inaweza kuwa bila mwezi au na miezi mingi. [[Dunia]] yetu ina mwezi moja tu. [[Mshtarii]] ina miezi zaidi ya 60, mingine mikubwa kama sayari ndogo mingine midogo yenye kipenyo cha 1 km tu. Utaridi haina mwezi.
 
Mwezi hauna nuru mwenyewe bali kunang'aa jwake kunatokana na nuru ya [[jua]] inaoakisiwa usoni mwake kama kwenye kioo.
 
'''Sayari yenye miezi''' katika [[mfumo wa jua]]:
* [[Dunia]]: mwezi mmoja
* [[Mirihi]]: miezi 2
* [[Mshtarii]]: miezi 63
* [[Zohali]]: miezi 31
* [[Uranus]]: miezi 27
* [[Neptun]]: miezi 13
* [[Pluto]]: miezi 3
 
'''Sayari zisizo na miezi''' katika mfumo wa jua:
* [[Utaridi]]
* [[Zuhura]] (Ng'andu)
 
[[Picha:Lunar libration with phase2.gif|thumb|right|200px|Mwendo wa mwezi]]
Mstari 30:
Huwa tunaangalia uso wake upande mmoja tene uleule tu. Sababu yake ni ya kwamba siku ya mwezi ni sawa na kipindi cha mwezi duniani. Mwezi unazunguka kwenye kipenyo chake katika muda wa siku 27.321 661 za dunia. Upande wa nyuma wa mwezi uko gizani wakati sisi tunaona mwezi mpevu. Wakati kwetu mwezi hauonekani upande wa nyuma unapokea nuru ya jua.
 
Uso wa mwezi unajaa mashimo ya [[kasoko]] yaliyosababishwa kwa kugongwa na [[meteoridi]]. Mwezi hauna angahewa inayozuia mapigo ya meteoridi ndogo au kupunguzu nguvu yao jinsi ilivyo duniani.
 
[[Picha:Earth Moon Scale.jpg|thumb|center|800px|Picha inayoonyesha umbali baina ya dunia na mwezi kulingana na ukubwa wao. Umbali wa wastani baina ya mwezi na dunia ni kilomita 384,400. Mwezi wetu una upana wa kilomita 3,470. Dunia yetu ina upana wa kilomita 12,800 <ref name="umbali_mwezi_dunia" />.]]
Mstari 36:
== [[Mwezi (wakati)]] kama kipimo cha wakati ==
[[Picha:Mond Phasen.jpg||framed|none|Awamu za mwezi kuanzia [[mwezi mwandamu]] kupitia robo ya kwanza, nusu mwezi, [[mwezi mpevu]], robo ya tatu hadi mwezi mwandamu tena]]
Uso wa mwezi jinsi unavyoonekana duniani hubadilikabadilika. Mwezi mpevu unaonekana kama duara kamili la kung'aa lakini baada ya kuonekana hivi umbo lapungua kila siku hadi kutoonekana kabisa na hali hii huitwa mwezi mwandamu. Baadaye mwezi unaonekana tena kama [[hilali]] nyembamba na kuongezeka hadi kuwa duara tena. Muda wa mabadiliko yote kupit mara 1 ni siku 29 1/4.
 
Muda wa mabadiliko kati ya mwezi mwandamu hadi kupotea na kuwa mwezi mwandamu tena ni kati ya siku 28 - 29. Kipindi hiki kinakumbukwa kirahisi, kinatazamiwa na watu wote wakati uleule kwa hiyo pamoja na kipindi cha siku kilikuwa kati ya vipimo vya kwanza vya wakati kwa binadamu.
 
Awamu za mwezi zilikuwa vipindi vya kuhesabu wakati tangu mwanzo wa kalenda. Hadi leo kuna [[kalenda ya mwezi]] ndiyo [[kalenda ya Kiislamu]] inayopanga wakati kutokana na hali halisi ya awamu za mwezi.
 
== Safari kwenda mwezini ==
Mstari 53:
 
Bila shaka ilhali hakujua haki za mali za Mjerumani katika mwaka 1980 Mwamerika Dennis M. Hope alifika mbele ya msajili wa viwanda mjini San Francisco akidai mwezi ni wake. Kufuatana na sheria ya Marekani kiwanda ni mali ya mtu akiandikisha dai lake na katika muda wa miaka minane hakuna upingamizi dhidi ya dai lake. Kwa njia hii -iliyowahi kufaulu tayari wakati wa karne zilizopita Wazungu walipojipata Amerika ya Kaskazini (hakuna aliyepinga madai yao mbele ya msajili)- alipata hati ya kumiliki akijaribu kuuza sasa mwezi polepole.
 
 
== Vyanzo ==
<references>
<ref name="umbali_mwezi_dunia">{{cite web | publisher=NASA | title="NASA Solar System Exploration: Planets" | url="http://solarsystem.nasa.gov/planets/profile.cfm?Object=Moon" | accessdate=2010-10-01 }}</ref>
</references>
 
 
 
{{mfumoMfumo wa jua na sayari zake}}
 
 
{{mbeguMbegu-sayansi}}
 
[[Jamii:Sayari]]