Zohali : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 164 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q193 (translate me)
No edit summary
Mstari 7:
 
Uso wa Zohali haionekani kwa sababu [[angahewa]] nzito inafunika kila sehemu. Mada ya angahewa ni hasa [[hidrojeni]]. Kutokana na uzito wa angahewa shindikizo ndani yake inaongezeka sana katika vilindi vyake na kusababisha [[gesi]] za angahewa kuingia katika hali ya [[giligili]] (majimaji) inayobadilika kuwa [[mango]] (imara) hadi [[metali]] ndani zaidi.
 
==Njia ya Zohali==
Zohali inazunguka jua kwa kutumia njia ambayo inakaribia kuwa na umbo la mviringo. <ref>njia za sayari nyingine hufanana zaidi na [[duaradufu]] </ref> Sehemu ambako inakaribia jua zaidi ([[periheli]]) ina umbali wa [[vizio astronomia]] 9.04, sehemu ambako ni mbali zaidi ([[afeli]]) ina umbali wa vizio astronomia 10.12.
 
Muda wa kumaliza njia ya kuzunguka jua ni miaka 29 na siku 166.
<ref>[http://nssdc.gsfc.nasa.gov/planetary/factsheet/saturnfact.html [[NASA]] "Saturn Fact Sheet"]</ref>
 
==Mzunguko wa sayari==
Zohali inazunguka kwenye mhimili wake katika muda wa takriban masaa 10 na nusu. Maanake siku ya Zohali ni fupi kuliko siku ya dunia yetu, chini ya nusu yake.
 
Kuna tofauti katika mkasi wa mzunguko huu kati ya kanda tofauti za Zohali. Kanda la [[ikweta]] linazunguka haraka zaidi kiasi kuhusu sehemu nyingine.
[[Picha:Muundo wa Zohali.png|250px|thumbnail|Muundo wa ndani wa sayari Zohali]].
 
Kanda la ikweta linazunguka katika muda wa masaa 10 na dakika 14, lakini maeneo yaliyo mbali na ikweta yanazunguka katika muda wa masaa 10 na dakika 38.
 
Hii inatokana na tabia za muundo wake kuwa mwili wa sayari hii imejengwa kwa gesi hasa [[hidrojeni]] inayopatikana kama hali ya gesi kwenye sehemu za nje na kiowevu katika tabaka za chini zaidi kwa hiyo sehemu kubwa ya masi yake si mango.
 
==Muundo wa sayari==
Zohali huhesabiwa kati ya sayari jitu za gesi yaani sarai kubwa sana zilizojengwa hasa kwa gesi inayopatikana katika hali mbalimbali kutokana na shinikizo kubwa inayotokea katika vilindi vyake.
 
Kipenyo cha Zohali ni takriban kilomita 120,000 na hii ni nafasi ya pili baada ya [[Mshtarii]] katika mfumo wa jua na sayari zake.
 
Masi yake ni ndogo kulingana na mjao wake: ina mjao wa 58% za Mshtarii lakini masi ni chini ya theluthi moja ya Mshtarii. Kwa hiyo [[densiti]] yake ni ndogo imekadiriwa kuwa 0.687 g/cm³ pekee.
 
Si rahisi kutofautisha kati ya angahewa ya sayari hii na uso wake kwa sababu sehemu kubwa ya "mwili" wa sayari ni gesi pia. Angahewa inayotazamiwa kwa nje ina kiwango kikubwa sana cha [[hidrojeni]] (96.3%) pamoja na kiasi cha [[heli]] (3.25%).
 
"Uso" wa sayari ni kanda ambako shinikizo ya [[kanieneo angahewa]] inafikia bar 1 (sawa na kanieneo angahewa duniani kwenye uwiano wa bahari).
 
Ndani zaidi hii shinikizo inaongezeka na kufanya gesi kuwa na tabia ya kiwevu.
 
Tena ndani zaidi kiwango cha shinikizo ni kubwa kiasi ya kwamba hidrojeni huwa manga na kuonyesha tabia za metali.
 
Chini ya tabaka ya hidrojeni metalia wataalamu huamini kuna kiini cha mwamba na barafu.
 
== [[mwezi|Miezi]] ya Zohali ==
Line 16 ⟶ 49:
Siku hizi imejulikana ya kwamba bangili ni vipande vya barafu, vumbi ba mawe. Vipande vyake vina ukubwa kati ya [[milimita]] chache hadi mita kadhaa kama motokaa. Unene wa bangili ni mita mamia kadhaa.
 
==Marejeo==
<references/>
 
{{commons|Saturn (planet)}}