Shirika kwa Ukoloni wa Kijerumani : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Kipala alihamisha ukurasa wa Shirika la Ukoloni wa Kijerumani hadi Shirika kwa Ukoloni wa Kijerumani: kusahihisha lemma
vichwa
Mstari 2:
'''Shirika kwa Ukoloni wa Kijerumani''' ([[jer.]] ''Gesellschaft für Deutsche Kolonisation'', GfdK; [[ing.]] ''"Society for German Colonization"'') lilikuwa shirika la binafsi nchini [[Ujerumani]] lililoweka msingi kwa [[koloni]] ya [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani]] katika eneo la [[Tanzania]] ya leo.
 
==Kuundwa na shabaha==
Shirika lilianzishwa tar 28 Machi 1884 na [[Karl Peters]] na Wajerumani wengi waliotaka Ujerumani kuingia kati ya mataifa yenye koloni. Shabaha ya shirika ilikuwa kuanzisha [[koloni]] za Kijerumani katika maeneo nje ya Ujerumani.
 
==Msafara wa Afrika ya Mashariki==
Baada ya kuundwa kwa shirika tume lake lilisafiri [[Zanzibar]] mwaka huohuo wa 1884 kwa shabaha ya kujipatia maeneo kwenye bara la Afrika. Wajumbe wa tume hili walikuwa Karl Peters, [[Joachim von Pfeil]] na [[Karl Jühlke]]. Kutoka Unguja Peters alivuka bahari akafika [[Saadani]]. Kutoka hapa aliendelea sehemu za ndani zaidi alipoanza kufahamiana na machifu katika [[Useguha]], [[Nguru]], [[Usagara]] na [[Ukami]] aliohamasisha kuweka alama zao kwenye karatasi zenye matini ya kuwa, walikabishi haki zao za kiutawala na kiuchumi kwa shirika. Kuna uhakika ya kwamba machifu wenyewe hawakuelewa maana ya karatasi hizi wala hawakuwa na madaraka yaliyopelekwa kwa shirika la ukoloni.
 
==Hati ya ulinzi na kuundwa kwa Kampuni ya kikoloni==
Baada ya kurudi Ujerumani mwaka 1885 Peters alitumia "mikataba" hii kwa kupata "hati ya ulinzi" ya serikali ya Ujerumani kwa ajili ya kazi ya shirika katika maeneo husika. Baada ya kupewa hati ya ulinzi Peters aliunda shirika mpya la [[Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki]] na kupeleka haki za shirika kuhusu maeneo ya Kiafrika kwake.