Christopher Mtikila : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
 
No edit summary
Mstari 1:
[[Image:Mtikila.jpg|right|thumb|Rev. Christopher Mtikila akihutubia mkutano wa hadhara. Picha kwa hisani ya [http://issamichuzi.blogspot.com/ Muhiddin Issa Michuzi]. ]]
Mchungaji Christopher Mtikila ni kiongozi wa chama cha upinzania [[Tanzania]] cha [[Democratic Party]] (DP). Mtikila alizaliwa Iringa, kusini mwa Tanzania, mwaka 1950. Pamoja na shughuli za siasa, Mchungaji Mtikila ni mwanzilishi na mkuu wa kanisa la kipentekoste la [[Full Salvation Church]]. Mchungaji Mtikila anajihusisha pia na harakati za haki za binadamu kwa kupitia kitengo cha haki za binadamu cha kanisa hilo kiitwacho [[Liberty Desk]]. Mwanzoni mwa miaka ya 90, mchungaji Mtikila alijipatia umaarufu mkubwa katika siasa za Tanzania kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuongea, upinzani wake dhidi ya muundo wa muungano kati ya [[Tanganyika]] na [[Zanzibar]], madai yake kuhusu uhujumu wa uchumi unaofanywa na wahindi (ambao anawaita Magabacholi), na kesi mbalimbali za kikatiba alizokuwa akifungua katika mahakama za Tanzania.