Majadiliano ya Wikipedia:Wakabidhi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 71:
 
:Usafiri wa kwenda Arusha au Moshi ungekuwa rahisi na basi, hasa Riverside Shuttle. Lakini hata Morogoro ingefikiwa rahisi, yaani tungeweza kuchukua ndege ya kwenda Dar halafu kuendelea na basi hadi Morogoro. Nimeangelia katika tovuti ya Opodo sasa hivi (http://www.opodo.com), na gharama ya ndege Nairobi-Dar na kurudi kwa mtu mmoja ni Euro 340. Kwa mfano, tukiondoka Ijumaa (tarehe 20 Machi) saa mbili za asubuhi, tutatua saa tatu na nusu huko Dar, tungepata basi ya Shabiby ya saa tano na kuingia Morogoro saa za mchana, kama saa nane au tisa. Halafu tukutane Ijumaa jioni na Jumamosi siku nzima, halafu tungeweza kurudi Jumapili (ndege ya mwisho kutoka Dar ni saa moja ya jioni). Tukikutana Arusha lakini nitajaribu kupanga uchunguzi mjini Magugu kwa mwezi wa Machi - halafu ningekuwa karibu zaidi. Wasalaam, --'''[[Mtumiaji:Baba Tabita|Baba Tabita]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Baba Tabita|majadiliano]])''' 13:28, 3 Desemba 2014 (UTC)
 
::Asante kwa utayari wa kuja Morogoro na kukutana na walimu wetu, si tu kwa kuuliza wanahitaji nini, bali pia kwa kuwahamasisha wachangie: wapo 40 hivi. Ila sipendi kulazimisha. Toka Dar kuna ndege pia kila siku kwenda na kurudi. Mkiamua, naweza kupeleleza bei. Kuhusu siku, napendelea pendekezo la Baba Tabita: Ijumaa jioni na Jumamosi nzima. Nakubali agenda za Kipala. Amani kwa wote! --'''[[Mtumiaji:Riccardo Riccioni|Riccardo Riccioni]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Riccardo Riccioni|majadiliano]])''' 12:49, 7 Desemba 2014 (UTC)
Return to the project page "Wakabidhi".