Hifadhi ya majadiliano kuhusu kubadilisha wakabidhi hadi mwaka 2019

Orodha ya Wakabidhi hariri

Wakabidhi wenzangu,

tunahitaji kupeleka ukaguzi wa orodha ya wakabidhi tena mbele ya jumuiya. Kabla ya kuitagangaza hatua hii naomba tuelewane kwanza kati yetu kuhusu mambo mawili

1. Nani atapiga kura kati ya wanawikipedia?

Pendekezo langu:

  • a) Mwenye kura awe aliyewahi kuandikishwa tangu mwezi 1 (hatutaki waliojiandikisha jana kwa kumpiga kura rafiki leo)
  • b) aliyewahi kuhariri makala 3 kwenye swwiki (nje ya ukurasa wake mwenyewe; hatukubali watu walioingia kwa kutunga/kusahihisha makala 1 pekee)
  • c) aliyehariri katika miezi 12 kabla ya kura yetu

Zamani tulikuwa wachache sana lakini siku hizi idadi ya waliojiandikisha imeongezeka ingawa wengi hawafanyi kitu tena, kwa hiyo tuelewane.

2. Kuhusu orodha ya wakabidhi kuna matatizo mawili:

a) tunaendelea kutunza majina ya wengine ambao ama hawakushiriki kabisa tangu miaka, au hawakushiriki katika shughuli za usimamizi. (hapa nitamwandikia kila mmoja na kumwuliza kama yuko tayari kutekeleza shughuli za admin: kupitia mara kwa mara ukurasa wa Mabadiliko ya Karibuni, kuangalia makala mpya na mabadiliko, kufuta spam dhahiri, kupeleka makala zisizofaa kwenye ukurasa wa ufutaji, kushiriki katika ufutaji, kukaribisha wageni) LAKINI tunahitaji watu zaidi walio tayari kufanya kazi hii

b) tuelewane nipeleke swali namna gani:

  • ama tufute tu wale wasioshiriki tena na kuchagua wapya wa nyongeza (wale wanaofanya kazi waendelee tu)
  • AU tufanye uchaguzi mpya kwa wote . Jambo hili si dhahiri na miradi ya wikipedia zinatofautiana hapa.

Naomba majibu kwenye ukurasa wa majadiliano ya wakabidhi. Kipala (majadiliano) 18:17, 23 Agosti 2020 (UTC)Reply

Pendekezo kuhusu kusitisha au kufuta wakabidhi hariri

Pendekezo langu kwa kura naona sasa hivi. Je inaweza kupelekwa vile?

  • Kama mkabidhi hakuhariri kabisa kwenye swwiki kwa mwaka mmoja, atajulishwa kwamba haki zake zitasitishwa karibuni;
  • asipojibu wala kurudi kuhariri, haki zake zitaondolewa;
  • kama alikuwa mkabidhi hai aliyetumia haki zake mara kwa mara anaweza kurudishwa kwa kibali cha wakabidhi hai wawili bila kura baada ya kuhariri tena katika swwiki kwa miezi mitatu Kipala (majadiliano) 18:38, 23 Agosti 2020 (UTC)Reply

Maoni yangu hariri

Nakubali mapendekezo ya Kipala. Kuhusu wakabidhi wanaofanya kazi sioni haja ya kupiga kura tena, lakini kwangu hakuna shida: niko tayari kuendelea na kazi au kuondolewa. Kuhusu kusitisha au kufuta wasiofanya kazi pendekezo la Kipala liwe kama sheria yetu ya kudumu: kimya cha mwaka mmoja kinatosha. Amani kwenu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 05:55, 24 Agosti 2020 (UTC)Reply

Hata mimi nakubali na kuwa tayari kwa kuendelea kazi yangu kama mkabidhi.ChriKo (majadiliano) 16:07, 24 Agosti 2020 (UTC)Reply
Niko nawe, ChriKo. Bado ninapenda kuendelea na kazi yangu. Mfano juzi tu, niliongeza idadi ya onyo katika makala kwa ufutaji dropdown menu! Laiti kama nisingekuwa na haki hiyo, basi ingebaki historia!--'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 06:06, 25 Agosti 2020 (UTC)Reply
Baba Tabita aliniandikia baruapepe (kwa Kijerumani) akiomba tumwondoe katika orodha ya wakabidhi. Kipala (majadiliano) 09:06, 31 Agosti 2020 (UTC)Reply
Habarini ndugu wakabidhi wenzangu.Nami pia nakubali kuendelea na ukabidhi.Nampongeza Kipala kwa kuendesha zoezi hili vizuri.Zaidi ya hayo nakubaliana na mapendekezo ya Kipala kuhusu kusitisha au kufuta wakabidhi kwa sababu ni mapendekezo ambayo hayajambana sana mtu, iwapo hakuwepo kwa mwaka mmoja kwa sababu mbalimbali, bado ana nafasi ya kuomba kurudi. Mwisho niwapongeze wakabidhi wote kwa kazi kubwa mnayoifanya ili kuijenga Wikipedia ya Kiswahili. Asanteni.--Jadnapac (majadiliano) 13:06, 4 Septemba 2020 (UTC)Reply
Nakubali kabisa pendekezo ka Kipala. Mwaka mmoja ni kipindi cha kutosha sidhani kama kuna mtu atalalamika kwa kufutwa. --Ndesanjo (majadiliano) 03:24, 1 Desemba 2020 (UTC)Reply

Maoni yangu hariri

chaguo lote ni sawa kwani wakabidhi ambao hawajatumia swwiki kwa muda watafutwa na pia wakabidhi ambao wamefikia kiwango cha kuwa wakabidhi wanapewa cheo cha kuwa mkabidhi

Mimi pia naona ni sawa kufuta ukabidhi baada ya kua kimya kwa mwaka mmoja. Pia tuwe na vigezo vya wazi vya nani anaweza kua mkabidhi, mafano, idadi ya michango au/pamoja na matumizi ya SW wikipedia Aneth (majadiliano) 07:36, 01 Desemba 2020 (UTC)Reply

Utaratibu wa kuzuia wanaoleta tafsiri ya kompyuta na kuandaa editathon ya kutafsiri makala hariri

Wakabidhi walipatana kwenye kikao cha tarehe 15. Agosti 2015:

1. Tunahitaji kudhibiti wachangiaji wanaotumia tafsiri ya kompyuta (ama google-translate au Wikipedia Content Translation) na kuunda makala zinazojaa matini isiyosafishwa. Makala hizo zinahatarisha hadhi ya wikipedia yetu na kuunda kazi nyingi kwetu wakabidhi na wanawikipedia wengine wanaosaidia kusahihisha.

Tulikubaliana kuhusu A) kuzuia wachangiaji wanaopakua matini kutoka tafsiri ya kompyuta bila masahihisho ya kutosha na
B) utaratibu wa kuendesha warsha au editathon ya kuunda makala kwa njia ya kutafsiri.

A.1. Kama mchangiaji amewekwa sanduku la “Karibu” (99%) ameshaona ni mwiko kumwaga matini ya tafsiri ya kompyuta. Kwa hiyo, kama anapakia matini ambayo ni tafsiri ya kompyuta yenye makosa atazuiliwa halafu tuweke alama za Kigezo:Zuia tafsiri kwenye ukurasa wake wa majadiliano. Ni alama hizo: {{Zuia tafsiri}} ~~~~. Kabla ya alama ya sahihi ~~~~ tunaweza kuongeza sababu za ziada.

A.2. Kila mkabidhi anayetumia njia hii anapaswa kuwezesha nafasi ya “Email this user”. Menginevyo tufuate maelezo kwenye Kigezo:Zuia tafsiri (https://sw.wikipedia.org/wiki/Kigezo:Zuia_tafsiri). Anaweza kukubaliwa tena akiahidi kusafisha makala zake.

B.1. Kuhusu mazoezi ya kuanzisha makala kwa njia ya warsha, editathon na kadhalika tusome na wote makala ya Msaada:Tafsiri. Tuwaonye wanaohudhuria wasitegemee programu za kutafsiri na watazuiliwa kama wanaleta matini yake moja kwa moja iliyobaki na kwa makosa ya lugha.

B.2. Katika zoezi la kundi tuwaeleze waunde makala zao katika nafasi ya mtumiaji (user space) kufuatana na maelezo katika Msaada:Tafsiri. Kila makala isomwe na kujadiliwa na jirani au mtu mwingine. Ikionekana haina kasoro za lugha, muundo wa sentensi, fomati ya viungo, interwiki, jamii na inaeleweka, basi inaweza kuhamishwa kwenye nafasi ya makala (article space). Kipala (majadiliano) 22:40, 17 Agosti 2021 (UTC)Reply

Return to the project page "Wakabidhi".