Nyigu : Tofauti kati ya masahihisho

148 bytes added ,  miaka 7 iliyopita
Nyongeza matini
(Ukurasa mpya)
 
(Nyongeza matini)
'''Nyigu''' ni [[wadudu]] wa [[nusuoda]] [[Apocrita]] katika [[oda]] [[Hymenoptera]] wasio [[nyuki]] au [[sisimizi]]. Wadudu hawa wote ni [[mbuai]] au [[kidusia|vidusia]] lakini ni [[lava]] tu ambao hula mawindo au mwathirika. Wadudu wapevu hula [[mbochi]], [[mbelewele]] au vitu vyingine vyenye [[sukari]]. Nyigu mbuai hukamata wadudu ([[kiwavi|viwavi]] mara nyingi) au [[arithropodi]] wengine. Huwaweka katika tundu ardhini au katika tundu lililoundwa kwa matope au kwa aina ya “[[karatasi]]” baada ya kuwapooza kwa [[sumu]] katika [[ganglioni]] kuu. Halafu nyigu hulitaga [[yai]] juu ya mdudu aliyekamatwa. Huyu aendelea kuwa hai na kwa hivyo lava wa nyigu akitoka kwenye yai anapata chakula kisichooza. Hata mdudu bila bahati afa tu akiwa ameliwa takriban kabisa. Jambo la nyigu vidusia linafanana lakini nyigu hawa huacha mwathirika ambapo alimpata. Hutaga yai au mayai juu au ndani yake na lava wakitoka kwenye mayai wanaanza kula mwathirika. Kwa sababu ya mwenendo huu nyigu vidusia hutumika sana kwa kufanya [[udhibiti wa kibiolojia]] dhidi ya visumbufu.
 
Kinyume na nyigu wengine spishi za [[familia (biolojia)|familia]] [[Chalcidae]] ([[nyigu-kidutu]]) husababisha vidutu kwa [[jani|majani]] ya [[mmea|mimea]] na lava hula tishu yao. Spishi jamaa za familia [[Agaonidae]] ([[nyigu-matini]]) huyataga mayai yao katika [[ovari]] za [[ua|maua]] ya [[mtini|mitini]].
 
==Picha==
11,961

edits