Content deleted Content added
Mstari 49:
 
Sehemu ya juu ya koti inafanana kikemia na ganda na sehemu hizi mbili zinaitwa tabakamwamba. Tabakamwamba ina unene wa kilomita 50 - 100. Tabakamwamba imekatika katika vipande vinavyoitwa [[mabamba la gandunia]]. Vipande hivi vinaelea juu ya giligili ya koti ya ndani. Hapo ni sababu ya kwamba bara si kitu cha milele; kila bamba huwa na mwendo wake na hapo ni sababu ya kwamba katika historia ya dunia mabara yameachana na kuungana. Kwa mfano imepimwa ya kwamba sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki ina mwendo wa kuachana na bara la Afrika na dalili yake ni bonde la ufa. Pale ambako mabamba yanapakana [[volkeno]] nyingi zinapatikana na [[matetemeko ya ardhi]] hutokea.
 
== Uga sumaku wa dunia ==
[[Picha:Magnetosphere rendition.jpg|350px|thumbnail|Mnururisho unavyotoka kwenye jua na kugengeushwa na mistari ya nguvu ya sumaku ya uga sumaku wa dunia]]
Dunia inazungukwa na [[uga sumaku]] yaani mistari ya nguvu ya [[kisumaku]]. Sababu yake ni ya kwamba [[kiini cha dunia]] inafanywa na [[chuma]] chenye tabia kama [[sumaku]] kubwa. Tabia hii inasababishwa na mwendo wa mikondo ya chuma cha moto kilichoyeyuka katika kiini cha nje cha dunia. Mistari ya nguvu ya sumaku inatoka nje kwenye ncha ya kusini na kurudi ndani ya dunia kwenye ncha ya kaskazini. Tabia hii ni msingi kwa kazi ya dira ambako sindano ya dira huvutwa daima na ncha sumaku ya dunia na kuelekea kaskazini muda wote.
 
Uga sumaku wa dunia ni kinga muhimu kwa uhai wote duniani. Dunia inapoke muda wote na mnururisho kutoa jua. Mnururisho uo ni nuru pamoja miale ya hatari. Uga sumaku unakengeusha sehemu kubwa ya mnururisho hatari hadi unapita kando la dunia na kutofika kwenye uso wa dunia.
 
== Dunia kama mahali pa maisha ==