Manii : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'Shahawa ni mbegu za mwanaume zinazohifadhiwa katika korodani.'
 
No edit summary
Mstari 1:
[[picha:sperm-egg.jpg|200px|thumb|Picha ya shahawa wakati inajaribu kuingia ndani ya yai ya kike]]
Shahawa ni mbegu za [[mwanaume]] zinazohifadhiwa katika korodani.
[[Picha:Espermatozoides.ogg|300px|thumbnail|Shahawa jinsi zinavyoonekana kwa hadubini]]
'''Shahawa''' ''([[ing.]] sperm, spermatozoon)'' ni mbegu za [[mwanaume]] zinazozalishwa katika [[korodani]]. Kila shahawa ni [[seli]] inayoweza kutembea nje ya mwili.
 
Kazi yake ni kubeba [[kromosomu]] zenye habari za [[jenetiki]] (yaani tabia za mwili inakotoka) na kufika kwenye [[uterasi]] ya kiumbe cha kike na kuingia huko ndani ya [[yai]]. Kuingia kwa shahawa ndani ya yai kunasababisha maungano ya [[DNA]] za yai na shahawa na ugawaji wa yai ambao ni chanzo cha kiumbe kipya.
 
Mfumo wa shahawa ni "kichwa" kidogo unachobeba DNA na mkia mrefu ambao mwendo wake unasogeza shahawa mbele. Umbo hili linafanana na [[kiluwiluwi]] mdogo lakini ni seli 1 tu.
 
Shahawa ya kibinadamu huzalishwa katika korodani ya mwanaume. Kila seli ya shahawa ina [[kromosomu]] 23. Binadamu huwa na kromosomu 46 kwa hiyo shahawa inabeba nusu ya habari zinazohitajika kwa kuanzisha kiumbe kipya. Nusu nyingine inapatikana katika yai ya kike ambako shahawa inaelekea kuingia.
 
Wakati wa tendo la ngono shahawa inafyatuliwa nje ya mboo wa kiume. Kama hii inatokea ndani ya kuma ya mwanamke shahawa inasambaa na kuenea ndani ya kuma. Ilhali idadi ya seli za shahawa ni kubwa sana ni seli mamilioni uwezekano ni mkubwa ya kwamba seli kadhaa za shahawa zinafika hadi uterasi na kukuta yai iliyo tayari. Si zaidi ya seli 100 kati ya milioni zilizotoka ambazo zinafika kwenye yai.
<ref name=analysis>{{citeweb|url=http://www.questdiagnostics.com/kbase/topic/medtest/hw5612/results.htm|title=SemenAnalysis Male Fertility Test, Sperm Count}}</ref>
 
Yai iliyo tayari inaweza kupokea seli 1 ya shahawa tu. Hapa kromosomu 23 ndani ya yai zinaunganishwa na kromosomu 23 za shahawa na hapa kuna jumla ya 46 zinazotosha kuanzisha kiumbe kipya.
 
==Marejeo==
<references/>
 
==Viungo vya Nje==
{{commons category|Spermatozoon diagrams}}
* [http://news.bbc.co.uk/2/hi/health/4529152.stm Slower conception 'leads to boys']
* [http://www.youtube.com/watch?v=vvnEsOaKxuw&NR=1 Human Sperm Under a Microscope]
 
 
[[jamii:mwili]]
[[jamii:jinsia]]