Tofauti kati ya marekesbisho "Unururifu"

731 bytes added ,  miaka 6 iliyopita
no edit summary
No edit summary
No edit summary
'''Unururifu''' ([[ing.]] ''radioactivity''; pia: '''mbunguo nururifu''' ing. ''radioactive decay'') ni tabia ya [[elementi]] kadhaa ambako [[kiini cha atomi]] si dhabiti bali inaweza kubadilika kuwa kiini cha atomi kingine na katika mchakato huu kinatoa [[mnururisho]]. Wakati wa badiliko atomi inatoa vyembe nyuklia. Mifano ya elementi ambazo si dhabiti ni [[urani]] na [[plutoni]].
 
Kuna pia hali za elementi kadhaa ambazo kwa kawaida ni thabiti lakini baada ya kupokea neutroni ya nyongeza zinakuwa nururifu. Kwa mfano kuna [[kaboni]] ya kawaida inayoitwa <sup>12</sup>C , hii ni thabiti. Lakini kuna pia kiwango kidogo cha <sup>14</sup>C ambayo si thabiti ni nururifu; hali hii huitwa [[isotopi]] cha kaboni. Kaboni ya <sup>14</sup>C inatengenezwa mfululizo katika tabaka za juu ya angahewa ya dunia ambako atomi za [[nitrojeni]] zinagongwa na miale ya jua na kupotea [[nyutroni]]; hizi nyutroni zinaweza kugongana tena na atomi ya nitrojeni na kujiunganisha naye na hivyo kuunda atomi ya <sup>14</sup>C.
Tabia hii ya unururifu ilitambuliwa mara ya kwanza na [[Antoine Henri Becquerel]] mwaka 1896, halafu ni [[Marie Curie]] na [[Pierre Curie]] waliotunga neno "radioactivity" (=unururifi) kwa tabia hii. Wote watatu walipokea [[Tuzo ya Nobel ya Fizikia]] kwa kazi hii mwaka 1903.
 
Mnururisho unaotoka wakati wa mbunguo nyuklia unatokea hasa kwa namna tatu zinazotajwa kwa herufi za Kigiriki [[alfa]], [[beta]] na [[gamma]] kuwa [[mnururisho α]], [[mnururisho β]] na [[mnururisho γ]]. Kati ya hizi kila moja inaweza kuwa hatari kwa binadamu na viumbehai kutegemeana na kiwango chake lakini hatuna [[mlango wa fahamu]] wa kuitambua.
Anonymous user