Mashariki ya Kati : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:MapRegionMiddleEast+Turkey.png|thumb|Mashariki ya Kati pamoja na [[Uturuki]].]]
'''Mashariki ya Kati''' ([[ing.]] ''Middle East'') ni namna ya kutaja sehemu kubwa ya [[Asia ya Magharibi]] pamoja na [[Afrika ya kaskazini-mashariki]], hasa [[Misri]].
 
Kwa kawaida nchi zifuatazo huhesabiwa humo:
Mstari 16:
* kuna namna mbalimbali za kutaja nchi za zaida zinazohesabiwa humo au la (kwa mfano: wengine huhesabu pia nchi za [[Asia ya Kati]] kama vile [[Kazakhstan]], [[Kyrgyzstan]], [[Tajikistan]] n.k.)
* jina ni tamko la Kiulaya: nchi hizi ziko upande wa [[mashariki]] kwa mtu aliyeko [[Ulaya]]. Kutoka Uswahilini ingekuwa zaidi "Kaskazini ya Kati"
* matumizi ya jina yamebadilika: zamani Kiingereza pamoja na lugha nyingine za Ulaya kilitofautisha kati ya
** "Mashariki ya Karibu" ''(Near East)'',
** "Mashariki ya Kati" ''(Middle East)'' na
Mstari 24:
** a) nchi za [[Bara Arabu]] na jirani;
** b) nchi za [[Uhindi]] na jirani
** c) nchi za [[Asia ya Mashariki]] kama China, Japani.
 
Lugha mbalimbali za Ulaya Bara kama [[Kijerumani]] zinaendelea kutumia majina haya matatu vile. Pia wataalamu wa [[historia]] kwa Kiingereza hupendelea kutofautisha kati ya "Mashariki ya Karibu" na "Mashariki ya Kati".
 
==Historia ya Mashariki ya Kati==
===Kitovu cha utamaduni na ustaarabu===
Nchi zinazoitwa kwa Kiingereza "Mashariki ya Kati" ziko kwenye eneo la dunia ambako watu na tamaduni za Asia, Afrika na Ulaya hukutana. Ni pia mahali ambako Bahari Hindi na Mediterenea zinakaribiana ambazo zote mbili zilikuwa njia za usafiri wa mbali tangu kale.
 
Pamoja na mahali pa kubadilishana bidhaa na teknolojia eneo hili lilikutanisha pia mawazo, falsafa na dini. Hadi leo Mashariki ya Kati ni kitovu cha kiroho cha dini za kama Uyahudi, Uislamu, Ukristo na Uzoroasta.
 
Idadi kubwa ya [[staarabu]] za kwanza duniani zilianza hapa kama vile [[Mesopotamia]] ([[Sumeri]], [[Akkad]], [[Assyria]], [[Babeli]]) na [[Misri ya Kale]], zikifuatwa na staarabu za Uajemi, Ugiriki ya Kale, Israeli ya Kale, [[Finisia]] na nyingine.
 
===Muhtasari wa historia ya utawala===
Eneo lote liliunganishwa mara ya kwanza chini ya [[Milki ya Ashuru]], halafu na [[milki ya pili ya Babeli]] iliyofuatwa na [[milki ya Uajemi]] na utawala wa [[Aleksander Mkuu]]. Baadaye eneo liligawiwa hasa kati ya milki mbalimbali za Uajemi na Dola la Roma hadi uenezaji wa Waarabu Waislamu na kuundwa kwa milki ya [[khalifa]]. Tangu 1512 Mashariki ya Kati karibu yote ilikuwa chini ya utawala wa [[Milki ya Osmani]] hadi [[Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia]].
 
===Ugawaji wa Milki ya Osmani===
Mashariki ya Kati ya kisasa yalianza kutokea baada ya vita hiyo. [[Ufaransa]] na [[Ufalme wa Maungano]] walishinda Milki ya Osmani wakagawana maeneo yao nje ya Uturuki. Ugawaji huu ulithebitishwa na [[Shirikisho la Mataifa]] na maeneo ya [[Syria]], [[Lebanoni]], [[Palestina]] (baadaye [[Israeli]] na [[Yordani]]) na [[Iraki]] yalikabishiwa kama [[maeneo ya kudhaminiwa]] kwa masharti ya kuyaandaa maeneo haya kuwa nchi huru baadaye.
 
Maeneo kadhaa kwenye rasi ya Uarabuni yalibaki huru baada ya kuondoka kwa jeshi la Osmani hadi mwaka 1918:
* Chifu Ibn Saud wa Riadh alishinda katika vita baina ya makabila ya Uarabuni ya kati akaweza kuvamia na kutawala maeneo ya Najd na Hejaz na mwaka 1932 alitangaza [[Ufalme wa Uarabuni wa Saudia]]
* Katika Yemen [[Imamu Yahya Muhamad]] wa kundi la [[Zaidiya]] alivamia velayat ya Yemen ya Kiosmani na kutangaza [[Ufalme wa Yemen]]
 
Uhuru ulifika kwa ngazi mbalimbali na tofauti kwa kila nchi.
 
'''Maeneo ya kudhaminiwa kwa Uingereza''':
*Iraki ilikubaliwa kuwa mwanachama wa Shirikisho la Mataifa mwaka 1932 ingawa hali halisi ilikuwa [[nchi lindwa]] chini ya athiri ya Uingereza hadi 1958.
*Palestina ng'ambo ya mto Yordani (Transjordan) ilipata serikali ya kujitawala kama nchi lindwa chini ya Uingereza tangu 1922, uhuru kamili 1946 kwa jina la Yordani.
*Israeli ilikubaliwa na Umoja wa Mataifa kuwa nchi huru mwaka 1948.
*Azimio lilelile lililenga kuanzisha pia dola la Kiarabu la Palestina lakii kutokana na vita iliyoanza mara moja hii haikutokea, maeneo yaliyotarajiwa kuwa Palestina yalivamiwa na Israeli, Yordani na [[Misri]]. Tangu 1993 kuna [[Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina]] yenye viwango tofauti vya utawala juu sehemu za maeneo ya Palestina asilia zilizo chini ya usimamizi wa kijeshi wa Israel.
 
'''Maeneo ya kudhaminiwa kwa Ufaransa''':
*Lebanoni ilitangaza uhuru wake mwaka 1943 wakati Ufaransa ulikuwa chini ya Ujerumani wakati wa [[Vita Kuu ya Pili ya Dunia]]
* Syria ilikuwa huru mwaka 1946
 
==Maeneo mengine baada ya Vita Kuu ya Kwanza==
Katika nchi kadhaa zilizokuwa nje ya Milki ya Osmani Uingereza ilikuwa na athira kubwa na hali halisi nchi hizi zilikuwa nchi lindwa kabla na baada ya Vita Kuu ya Kwanza
* [[Misri]] ilikuwa rasmi sehemu ya Milki ya Osmani lakini hali halisi ilisimamiwa na Uingereza hasa kwa shabaha ya kusimamia [[mfereji wa Suez]]. 1914 ilitangazwa kuwa nchi lindwa chini ya Uingereza; tangazo la uhuru la 1922 bado iliacha athira kubwa kwa Uingereza. Tangu 1952 Misri imepata uhuru kamili, na tangu ilitawala pia mfereji wa Suez.
*[[Omani]] ilikuwa eneo lililogawiwa kati ya [[Sultani wa Maskat]] na [[Imamu wa Ibadiya]] mnamo 1890. Maskat ilikubali kuwa eneo lindwa chini ya Uingereza ikapata msaada wa jeshi la Uingereza dhidi ya Saudia na baadaye kuvamia na kutawala pia maeneo ya imamu 1957. Mkataba wa 1951 ulitangaza uhuru wa Omani lakini hali halisi athira ya Uingereza ulikuwa na nguvu hadi miaka ya 1990s.
* [[Kuwait]] ilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza tangu 1899 na Waingereza walitetea hali yake ya pekee dhidi ya Waosmani na baadaye dhidi ya Saudia. Ilipata uhuru mwaka 1961.
* Maeneo ya [[Falme za Kiarabu]] pamoja na [[Qatar]] na [[Bahrain]] yalikuwa nyumbani kwa makabila madogo na chifu zao. Tangu 1820 walikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na [[uharamia]] na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzo huu ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20. Tangu 1971 madola haya madogo yalipata uhuru. Saba kati yao yaliungana kuwa Falme za Kiarabu.
 
==Ugunduzi wa mafuta==
Katika karne ya 20 mafuta ya petroli yaligunduliwa kwanza katika Uajemi, badaye pia katika nchi nyingine. Mafuta yalibadilisha umuhimu wa Mashariki ya Kati. Maffuta ya petroli iliendelea kuwa chanzo muhimu zaidi cha nishati katika uchumi wa dunia ya kisasa. Uingereza na baadaye hasa Marekani walijaribu kuhakikisha ya kwamba serikali za nchi zenye mafuta ziko upande wao.
 
Baada ya 1945 mapato kutokana na mafuta yalianza kubadilisha maisha na jamii za nchi zote zinazouza mafuta kwenye soko la dunia. Hasa watawala wa nchi ndogo walikuwa matajiri kupita kiasi wakaweza kuendelea na mfumo wa utawala wa mfalme asiyebanwa na katiba kwa muda mrefu kwa sababu waliweza kuwagawia wananchi wao sehemu za utajiri wa mafuta.
 
Wakati wa [[vita baridi]] mashindano kati ya magharibi na Umoja wa Kisovyeti yaliedeshwa vikali katika Mashariki ya Kati. Serikali mbalimbali zilichezacheza kati ya pande mbili.
 
 
 
==Viungo vya nje==