Mnyoo-bapa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa mpya
 
dNo edit summary
 
Mstari 20:
'''Minyoo-bapa''' ni [[mnyama|wanyama]] wanaofanana na [[mnyoo|minyoo]], lakini wao hawana [[uwazi wa mwili]] ([[w:coelom|coelom]]). Kwa hivyo hawana [[ogani]] za [[mfumo wa mzunguko wa damu]] au za [[mfumo wa upumuaji]] na lazima [[mwili]] uwe bapa ili [[oksijeni]] iweze kuingia kwa mtawanyiko. Mwili wao una uwazi umoja, ule wa [[mmeng'enyo]], lakini uwazi huu una kipenyo kimoja tu pamoja kwa umezaji na kwa utoaji.
 
Kuna minyoo-bapa ambao huishi kwa maji au kwa udongo. Kwa kawaida hawa hula wanyama wadogo lakini pia wanyama wakubwa kuliko wao wenyewe, kama [[konokono]]. Zaidi ya nusu ya spishi zote za minyoo-bapa ni [[kidusia|vidusia]], k.m. [[tegu|mategu]]. Hawa hufyonda virutubishi vilivyoyeyuka katika giligili za mwili wa mwenyeji.
 
==Picha==