VIPENGELE VYA FASIHI SIMULIZI : Tofauti kati ya masahihisho
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'Fasihi ndiyo aina pekee ya sanaa inayotumia lugha kujitambulisha au kujitofautisha na aina nyingine za sanaa. fasihi zipo za aina mbili,nazo ni 1*Fasihi simuli....' |
(Hakuna tofauti)
|
Pitio la 13:06, 8 Oktoba 2016
Fasihi ndiyo aina pekee ya sanaa inayotumia lugha kujitambulisha au kujitofautisha na aina nyingine za sanaa. fasihi zipo za aina mbili,nazo ni 1*Fasihi simuli. 2*Fasihi andishi.
FASIHI SIMULIZI
Fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mazungumzo ya mdomo ili kufikisha ujumbe kwa hadhira.Aina hii ya fasihi ndiyo iliyokuwapo tangu zamani kabisa mwanadamu alipoanza kuishi yaani ilianza pale mwanadamu alipochangamana na wenzake katika kufanya mambo mbalimbali mfano,shughuli za biashara,kilimo,na nyinginezo.
AINA ZA FASIHI SIMULIZI
Utanzu huu wa fasihi una vipera au aina kuu nne,nazo ni 1*Hadithi. 2*Ushairi. 3*Semi. 4*maigizo.
SEMI
Semi ni tungo fupi za kisanaa zitumiazo picha na tamathali kuelezea maudhui yanayobeba mafunzo ya kijamii.
TANZU ZA SEMI
Semi ina vipera au tanzu sita ambazo ni, 1*Methali 2*Vitendawili 3*Nahau 4*Misemo 5*Mafumbo 6*Mizungu
METHALI
Methali ni semi fupi zenye mpangilio maalumu wa maneno ambazo huelezea kwa muhtasari mafumbo na mawazo mazito yanayotokana na uzoefu wa kijamii. Methali huundwa na vipande viwili vya maneno vyenye fikra yurani.Kipande cha kwanza huashilia tendo au sharti na kipannde cha pili huashilia matokeo ya tendo au sharti hilo. Mfano wa methali 1*Mcheka kilema,hali hakija mfika. 2*Kupotea njia, ndiko kujua njia. 3*Mchelea mwana kulia, utalia wewe. Maana ya methali hutegenea muktadha au wakati maalumu kati jamii.
KAZI ZA METHALI
Methali zina kazi nyingi katika jamii yoyote ile kama vile, 1*Kuionya jamii inayohusika au inayopewa methali hiyo. 2*Kuishauri jamii inayopewa au kutamkiwa methali hiyo. 3*Kuihiza jamii inayohusika. 4*Kukejeli mambio mbalimbali yanayofanyika ndani ya jamii husika.