Ncha ya kijiografia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'Picha:Earth's_Axis_(small).gif|350px|thumbnail|Dunia inazunguka kwenye mhimili wake inayoonyeshwa kwa mstari mweupe. Ncha iko mahali ambako mstari huu unapita...'
 
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:Earth's_Axis_(small).gif|350px|thumbnail|Dunia inazunguka kwenye mhimili wake inayoonyeshwa kwa mstari mweupe. Ncha iko mahali ambako mstari huu unapita uso wa dunia. Picha hii inatazama dunia kwa upande hivyo ni ncha ya kaskazini pekee inayoonekana]]
 
'''Ncha ya kijiografia''' ni moja kati ya mahali pawili ambako mhimili wa mzunguko wa [[dunia]] unakutana na uso wa dunia. Kwa maana hii ncha zinapatikana pia kwenye [[sayari]], [[mwezi]] au [[gimba la angani]] kubwa nyingine linalozunguka kwenye mhimili wake.
 
Ncha mbili kwa kawaida hutofautishwa kwa kuziita ama "[[ncha ya kaskazini]]" au "[[ncha ya kusini]]" jinsi ilivyo kwenye dunia yetu. Kila ncha iko kwa [[nyuzi]] 90 kutoka mstari wa [[ikweta]].
 
Kwenye magimba ya angani kama dunia yetu kuna mabadiliko madogo ya mara kwa mara kwenye mzunguko wa sayari. Haya yanasababisha ncha kuhama kidogokiasi mara kwa mara. Kwa hiyo mahali kamili pa ncha za dunia huhama mita chache kila mwaka. Ramani na data za kijiografia hutumia wastani kati ya mahali pale.
 
Kama gimba la angani lina [[uga sumaku]] kuna pia ncha sumaku. Kwa dunia yetu mhimili wa uga sumaku iko karibu na mhimili wa mzunguko na kwa hiyo ncha sumaku na ncha jiografia ziko tofauti lakini karibu. Lakini hii si lazima kwa kila sayari. Kwenye sayari [[Uranus]] kuna tofauti wa nyuzi 60°.
 
==Tazama pia==