Mohammed Abdelaziz ni katibu mkuu wa Polisario na rais wa Jamhuri ya Sahara ya Kidemokrasia ya Kiarabu inayodai kuwa dola la Sahara ya Magharibi.

Mohamed Abdelaziz, picha ya mwaka 2000

Alikuwa kati ya viongozi wa kwanza wa Polisario iliyopigania uhuru wa Sahara ya Magharibi. Alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Polisario mwaka 1976 halafu pia rais wa serikali ya Jamhuri ya Sahara. Anaishi katika kambi la wakimbizi la Tindouf (Algeria).

Mohammed Abdelaziz kama kiongozi alikubali njia ya mazungumzo na diplomasia. Alihakikisha ya kwamba vita ya Polisario ilikuwa "vita" safi bila kutumia mbinu za ugaidi. Ana wapinzani wake wanaopendelea kurudi vitani dhidi ya Moroko. Amehakikisha