Sahara ya Magharibi

الجمهورية العربية الصحراوية الديمقراطية
Al-Jumhūrīyâ al-Arabīyâ as-Sahrāwīyâ ad-Dīmuqrātīyâ
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahara

Sahara ya Magharibi
Bendera ya Sahara ya Magharibi Nembo la Sahara ya Magharibi
(Bendera) (Nembo)
Lugha rasmi Kiarabu na Kihispania
Mji mkuu El Aaiún
Mji mkubwa El Aaiún
Rais
(wa nje)
Mohamed Abdelaziz
Waziri Mkuu (wa nje) Abdelkader Taleb Oumar
Eneo
 - Jumla
 - % maji

266 000 km²
--
Wakazi
 - Jumla
 - Msongamano wa watu

548,000 (Julai 2003)
1/km²
Uhuru
 - ilitangazwa
 - Nchi kutwaliwa
na Hispania
  27 Februari 1976
 na Moroko
Pesa Dirham ya Moroko
Wakati UTC 0
Wimbo la taifa ?
TLD (mtandaoni) -- (.eh iliwekwa tayari)
simu ya kimataifa + 212. (kama Moroko)

Sahara ya Magharibi ni eneo la Afrika ya Kaskazini-Magharibi kwenye mwambao wa Bahari Atlantiki upande wa magharibi.

Ramani ya Sahara ya Magharibi

Imepakana na Moroko upande wa kaskazini, Algeria upande wa mashariki na Mauretania upande wa kusini.

Ilitangazwa nchi huru mwaka 1976 kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahara lakini kwa kiasi kikubwa inatawaliwa na Moroko kama mikoa yake ya kusini.

Nchi nyingi za dunia pamoja na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika hazitambui Sahara Magharibi kuwa sehemu ya Moroko. Nchi 53 zinaikubali kama Jamhuri huru. Hali halisi sehemu kubwa ya ardhi yake inatawaliwa na Moroko inayodai ni sehemu ya eneo lake la kitaifa.

Sehemu kubwa ya wakazi asilia wako nje ya eneo kama wakimbizi katika makambi makubwa nchini Algeria.

Historia

hariri

Kabla ya ukoloni

hariri

Sahara ya Magharibi haikuwahi kuwa dola la pekee katika historia yake. Wakazi walikuwa wachache kwa sababu eneo lote ni jangwa. Kuna kilimo kidogo tu katika oasisi.

Wakazi wake walikuwa wa makabila ya Waberber waliochanganyika na Waarabu tangu uvamizi wa Kiislamu.

Ndilo eneo la asili la Wamurabitun waliojenga utawala juu ya Moroko, Hispania na sehemu kubwa ya Afrika ya Kaskazini hadi mipaka ya Misri na Senegal mnamo karne ya 11 BK.

Koloni la Hispania

hariri

Mwaka 1884 Hispania ilichukua utawala wa maeneo ya pwani na kuyatangaza kuwa koloni lake kwa jina la "Sahara ya Hispania". Ilivutwa hasa na malighafi za fosfeti.

Tangu mwaka 1973 wanaharakati ya kupigania uhuru wa Polisario walipigana na jeshi la Wahispania. Wakati uleule dikteta wa Hispania Francisco Franco aligonjeka kabla ya kifo chake. Serikali yake ilianza majadiliano na Polisario kuhusu uhuru lakini majirani yake, Moroko na Mauretania, walidai ya kwamba koloni la Hispania lingestahili kuwa sehemu ya maeneo yao.

Moroko iliomba usaidizi wa Mahakama ya Kimataifa yalioamua tarehe 16 Oktoba 1975 ya kwamba hakuna haki za Moroko juu ya Sahara ya Magharibi na azimio lolote kuhusu hali ya eneo linapaswa kuamuliwa na wenyeji wenyewe.

Wakati huohuo tume ya Umoja wa Mataifa ilitembelea Sahara ya Magharibi likatoa taarifa ya kwamba wananchi walitaka uhuru.

Mfalme Hassan II wa Moroko aliongeza shinikizo mnamo Novemba 1976 kwa kutuma mpakani wananchi Wamoroko 350.000 wasio na silaha waliovuka mpaka kidogo wakati wanajeshi Wahispania hawakufyatulia risasi.

Siku chache baada ya kifo cha Franco Wahispania waliamua kuondoka katika matatizo haya. Walifanya mapatano na Moroko na Mauretania bila kushauriana na wananchi wenyewe ili Moroko ichukue sehemu ya kaskazini na Mauretania sehemu ya kusini ya koloni.

Mnamo Desemba 1975 Wahispania waliondoka. Wanajeshi Wamoroko waliingia na Polisario ilitangaza Jamhuri ya Sahara ya Kidemokrasia ya Kiarabu mwanzo wa 1976.

Polisario ilipigania uhuru

hariri

Huu ulikuwa mwanzo wa vita vya miaka mingi. Polisario ilishambulia wavamizi waliokuwa na nguvu tofauti: jeshi hafifu la Mauretania na jeshi lenye nguvu na silaha za kisasa la Moroko.

Idadi kubwa ya wananchi walikimbia wakapewa makambi katika Algeria ya kusini walipoweza kujitawala. Algeria ilikubali Jamhuri ya Sahara na kuwaruhusu Polisario kutumia makambi kama vituo vya kijeshi dhidi ya Moroko.

Polisario ilifaulu kushinda jeshi la Mauretania hata walishambulia mji mkuu wa Nuakshott. Waarabu wengi wa Mauretania waliunga mkono wenzao wa Sahara ya Magharibi.

Mwaka 1979 Mauretania iliondoka kabisa katika Sahara ya Magharibi, lakini Wamoroko waliingia na kuteka eneo lote.

 
Maeneo ya Sahara ya Magharibi ya kuzungukwa na ukuta wa Moroko; njano ni eneo nje ya utawala wa Moroko

Vita vilikuwa vigumu kwa sababu Polisario haikuwa na uwezo wa kushinda jeshi lenye silaha za kisasa kabisa, lakini Wamoroko walishindwa vilevile kuwazuia Polisario wasiingie mara kwa mara na kupita makambi ya jeshi la Moroko na kushambulia vituo vyao kwa vikundi vidogo.

Hapo Moroko ilianza kujenga ukuta na vizuizi jangwani kwa urefu wa km 2,720 vinavyoacha sehemu ndogo ya jangwa mikononi mwa Polisario na sehemu zenye vijiji na miji mikononi mwa Moroko.

Eneo lililogawiwa

hariri

Vita vimesimama tangu mwaka 1991 kufuatana na mapatano kati ya Moroko, Polisario na Umoja wa Mataifa. Kura ya wananchi kuhusu suala la uhuru ilikubaliwa. Kura hiyo ilitakiwa kufanyika mwaka 1992 lakini imeshindikana hadi leo kwa sababu Moroko na Polisario hawakubaliani ni nani mwenye haki ya kupiga kura. Polisario ilikataa wakazi wengi waliohamia kutoka Moroko wasipige kura; Moroko ilitia wasiwasi ya kwamba wakazi wengi wa makambi huko Algeria si wenyeji wa Sahara ya Magharibi hivyo wasipige kura.

Moroko imeendelea kupeleka raia zake ili wajenge nyumba katika Sahara ya Magharibi. Idadi yao imeshapita idadi ya wenyeji waliobaki ndani ya maeneo chini ya Moroko.

Tazama pia

hariri


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sahara ya Magharibi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.