Wilaya ya Karonga ni wilaya mojawapo katika Kanda ya Kaskazini ya Malawi. Wilaya ina eneo la km² 3,355. Idadi ya wakazi ni 365,028. [1]

Mahali pa Wilaya ya Karonga nchini Malawi
Mahali pa Wilaya ya Karonga nchini Malawi

Ni wilaya ya mpakani kati ya Malawi na Tanzania, inayokaliwa zaidi na Wankhonde na matawi mengine ya Wanyakyusa.

Barabara kuu kutoka Tanzania hadi Malawi inapita mpaka katika kazkazini ya wilaya, kwenye kituo cha Songwe.

Makao makuu ya wilaya yapo Karonga mjini.

Uchumi hariri

Katika miaka michache iliyopita, kumekuwa na maendeleo mengi katika wilaya hii kutokana na ugunduzi wa urani katika mgodi wa Kayelekera, uliofunguliwa rasmi mwaka 2009. Barabara nyingi za awali zilizokuwa na changarawe zimewekwa lami.

Utalii hariri

Kuna hoteli nyingi na nyumba za wageni huko Karonga, kando ya Ziwa Nyasa (inayoitwa hapa Ziwa Malawi) .

Mgawanyiko wa serikali na utawala hariri

Kuna majimbo bunge matano wilayani:

  • Karonga - Kati
  • Karonga - Kaskazini
  • Karonga - Kaskazini Magharibi
  • Karonga - Nyungwe
  • Karonga - Kusini

Tangu uchaguzi wa 2009 Karonga Nyungwe imewakilishwa na mwanasiasa wa AFORD, na viti vingine vinashikiliwa na wanachama wa Democratic Progressive Party . [2]

Marejeo hariri

  1. "2018 Population and Housing Census Main Report". Malawi National Statistical Office. Iliwekwa mnamo 25 December 2019.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Parliament of Malawi - Members of Parliament - Karonga District". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-17. Iliwekwa mnamo 2011-01-19.