Kanda ya Kaskazini, Malawi

Kanda ya Kaskazini ni kanda ya kiutawala nchini Malawi. Mnamo mwaka 2018 ilikuwa na wakazi 2,289,780[1] katika eneo la km² 26,931.

Eneo la Kanda ya Kaskazini nchini Malawi

Makao makuu yako mjini Mzuzu. Kanda ya Kaskazini inapakana na Tanzania, Ziwa Nyasa, Kanda ya Kati na Zambia .

JiografiaEdit

Kati ya wilaya 28 nchini Malawi, sita ziko ndani ya Mkoa wa Kaskazini.

Mbali na sehemu za Malawi bara, Mkoa wa Kaskazini pia unajumuisha visiwa vya Chizumulu na Likoma katika Ziwa Nyasa, ambavyo kwa pamoja vinaunda Wilaya ya Likoma.

MarejeoEdit

  1. Malawi Regions, tovuti ya citypopulation.de