Seattle, Washington
Seattle ni mji katika jimbo la Washington (ncha ya magharibi na kaskazini ya Marekani). Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2007, mji una wakazi wapatao milioni 3.3 wanaoishi katika mji huu. Mji upo m 0-158 kutoka juu ya usawa wa bahari.
Jiji la Seattle | |
Nchi | Marekani |
---|---|
Jimbo | Washington |
Wilaya | King |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 594,210 |
Tovuti: www.seattle.gov |
Seattle ni bandari ya uziwa. Seattle na Mombasa (Kenya) ni miji-ndugu.
Seattle ni mji mkubwa zaidi ya miji yote katika jimbo la Washington na mkoa wa Pacific Northwest katika Marekani Kaskazini. Mji wa Seattle una idadi ya watu ya milioni 3.87 na mji huu ni kubwa zaidi ya kumi na tano katika Marekani, kutoka mujibu wa sense iliyofanyika mwaka 2018. Katika Julai 2013, Seattle iliongeza haraka zaidi katika miji mikuu ya Marekani.
Mji upo ismus kati ya Puget Sound (njia ya Bahari ya Pasifiki) na Ziwa Washington, maili 100 (160 km) kusini mwa mpaka wa Marekani na Canada. Seattle ni njia kuu ya biashara kati ya Marekani na Asia. Mji una bandari ya nne kwa ukubwa katika Marekani Kaskazini kwa kontena, tangu mwaka 2015.
Wamarekani wa asili walikaa eneo la Seattle si chini ya miaka 4,000 kabla ya wakoloni wazungu kuja kwa mara ya kwanza. Arthur A. Denny na kundi la wazungu, ambalo liliitwa “Denny Party,” walifika Alki Point tarehe 13 Novemba, 1851 katika meli inayoitwa Exact. Walitoka Illinois na walipitia Portland, Oregon kabla ya kufika eneo la Seattle. Walianzisha koloni katika pwani ya mashariki ya Elliott Bay ambayo waliita “Seattle” mwaka 1852 kuheshimu Mtemi Si’ahl wa makabila ya huko yaliyoitwa Duwamish na Suquamish. Sasa, Seattle ina idadi kubwa ya watu kama wamarekani wa asili, waafrika na waasia. Pia, ni mji wa sita kwa kuwa na idadi ya watu wa jamii ya LGBT katika Marekani kwa asilimia.
Kiwanda kikuu cha kwanza katika Seattle kilikuwa kukata mbao. Lakini, mwishoni mwa miaka 1800, mji ulibadilika na ulikuwa kituo kikubwa cha biashara na mahali pa kutengenezea meli. Seattle ilikuwa njia kwa watu waliosafiri Alaska wakati wa Klondike Gold Rush. Baada ya vita ya pili ya dunia, Seattle ilikuwa kituo cha kutengenezea ndege, kwa sababu shirika la Boeing lilianzishwa hapo. Tangu miaka ya 80, Seattle imekuwa kituo cha teknolojia na makampuni kama Microsoft na Amazon, ambayo yalianzishwa hapo. Kampuni ya ndege ya Alaska Airlines ilianzishwa katika SeaTac, Washington na ilihudumia uwanja wa ndege wa Seattle, Seattle-Tacoma International Airport. Mji umeona ukuaji wa uchumi kwa sababu makampuni mapya ya teknolojia na mtandao yalileta fedha na rasilimali. Idadi ya watu iliongezeka kwa 50,000 kati ya miaka 1990 na 2000. Seattle na jimbo la Washington lina baadhi ya mishahara mikuu zaidi katika nchi – $15 kwa saa kwa biashara ndogo ndogo na $16 kwa makampuni makuu – kwa sababu idadi ya watu wanaongezeka haraka sana.
Seattle ina historia muhimu ya muziki pia. Kati ya miaka ya 1918 na 1951, kulikuwa na karibu vilabu ishirini na nne vya klabu muziki wa jazz katika mtaa wa Jackson, kutoka wilaya ya Chinatown/International mpaka wilaya ya katikati. Seattle ni mahali pa kuzaliwa ya mwanamuziki maarufu, Jimi Hendrix, na pia makundi ya Nirvana, Pearl Jam, Foo Fighters na harakati za muziki wa mwamba mbadala.
Uchumi
Mji umejulikana kimataifa hasa kwa sababu hadi 2001 ilikuwa makao makuu ya kampuni ya Boeing inayojenga ndege za abiria na mizigo.
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Seattle, Washington kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |