Boeing
kampuni ya kutengeneza ndege nchini Marekani
Boeing ni kampuni nchini Marekani ya kutengeneza eropleni, helikopta, roketi na vifaa vingine kwa matumizi ya kiraia na ya kijeshi kwa usafiri wa hewani na kwenye anga-nje. Ni kampuni kubwa duniani ya aina hii; katika utengenezaji wa ndege za abiria pekee ina nafasi ya pili baada ya Airbus ya Ulaya.
Makao makuu ya kampuni yalikuwepo Seattle, Washington lakini tangu 2001 yalihamishwa kwenda Chicago.
Modeli za Boeing zinazojulikana sana ni pamoja na
- Boeing 707 (haitengenezwi tena)
- Boeing 717 (haitengenezwi tena)
- Boeing 727 (haitengenezwi tena)
- Boeing 737 (iliyotengenezwa mara nyingi kushinda modeli zote)
- Boeing 747 (inajulikana kama 'Jumbo Jet')
- Boeing 757 ((haitengenezwi tena))
- Boeing 767
- Boeing 777 (inajulikana pia kama "Triple Seven")
- Boeing 787 (inajulikana pia kama "Dreamliner")
- Boeing F/A-18 Hornet
- Boeing F-15 Eagle
- Boeing KC-135 Stratotanker
- Boeing X-37 (inajulikana kama orbital test vehicle) imezinduliwa tarehe 22 Aprili 2010.