Mabantu
"Mabantu" ni jina la kutaja kundi la muziki wa Bongo Flava kutoka jijini Dar es Salaam, Tanzania.[1] Kundi linaundwa na wasanii wawili, Twarha Kanengo (Twarha Mabantu-9 Julai, 1997) na Mwarami Kajonje (Muuh Mabantu-21 Januari, 1999).
Mabantu | |
---|---|
Twaah (aliyesimama) na Muuh Mabantu (aliyechutuma) wakiwa katika seti ya Tamasha la Nandy—2021. | |
Taarifa za awali | |
Kazi yake | Wanamuziki |
Miaka ya kazi | 2018 |
Ameshirikiana na | Whozu, Young Lunya, R the DJ |
Kwa pamoja, wanafahamika kwa wimbo wao Sundi (2018), Bodaboda (2018) "Kama Tulivyo" (2019) wakimshirikisha Whozu[2], na ule maarufu zaidi ni Nawakera walishirikiana na Young Lunya. Pia waliwahi kufanya kazi ya kishirikishi na R "the" DJ, Shobo (2021).
Mabantu walikuja kutambulika zaidi kupita kiasi baada ya kutoa Sponsa (2020), walirudi tena na Young Lunya.
Historia
haririHapo awali, wawili hawa wote walikuwa katika taasisi ya Said Fella, maarufu kama "Mkubwa na Wanawe" wakiwa sehemu ya wasanii wanaosubiri kuwezeshwa. Ilipotimu mnamo mwaka wa 2013, kabla hata ya kushiriki katika wimbo hata mmoja, vijana hawa waliamua kuondoka mikononi mwa mkubwa na wanawe, na hatimaye kuanzisha Mabantu rasmi.
Mwarami aliingia Mkubwa na Wanawe mwishoni mwa 2011, wakati Twarha aliingia 2012 mwishoni. Lakini lilipokuja suala la kutaka kujiendeleza zaidi nje ya mikono ya kituo cha Mkubwa Fella, iliwalazimu waje na jina la kundi ambalo wangelitumia kama utambulisho kwa wasanii hawa.
Wakiwa kituoni kwa Fella, walipata fursa ya kushiriki mazoezi mbalimbali ya kuondoa uwoga wa hadhira na matumizi ya ala za sauti na vyombo vya muziki. Kituo kilikuwa na kila aina ya vifaa wezeshi kwa watoto wanaokaa hapo. Walirekodi nyimbo kadhaa ambazo hazikutoka nje ya kituo hicho. Kimsingi, Twarha ni mnenguaji na mwimbaji, wakati Mwarami alijipambanua kama mwimbaji zaidi.
Nyimbo maarufu
haririHizi ni baadhi ya nyimbo za Mabantu.
Na. | Jina la wimbo | Maelezo |
---|---|---|
1. | Umenuna | |
2. | Hachiti | |
3. | Nawakera | |
4. | No Love No Stress | |
5. | Show Show | |
6. | Sina Shida Nae | |
7. | Happy Birthday | |
8. | Mguu Pande | |
9. | Mwendo | |
10. | Amina |
Marejeo
hariri- ↑ "EXCLUSIVE: Tazama Mabantu wakichambua mistari ya wimbo wa 'Sundi' – Dar24" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-10-02.
- ↑ "Mabantu wafunguka kuhusu Whozu kukatwa nywele | East Africa Television". www.eatv.tv. 2019-03-26. Iliwekwa mnamo 2021-10-02.