Madini silikati
Madini silikati ni madini yanayounda miamba mbalimbali. Yote yanaundwa na anioni zenye silikoni na oksijeni. Ndilo kundi kubwa na muhimu zaidi katika madini yote likifanya karibu asilimia 90 za ganda la Dunia. [1] [2] [3]
Silika (dioksidi ya silikoni) SiO2 kawaida huhesabiwa kuwa madini silikati. Silika hupatikana katika maumbile kama shondo na maumbo yake.
Muundo wa jumlaEdit
Madini silikati kimsingi ni kampaundi ya ioni ilhali anioni zake huwa na atomi za silikoni na atomi za oksijeni.
Katika madini mengi kila atomi ya silikoni iko katikati ya kitovu cha piramidi pembetatu (tetrahedron), ambako pembe zake ni atomi za oksijeni nne.
Kikundi kikuu | Muundo | Fomula | Mfano |
---|---|---|---|
Nesosilikati | pekee ya silicon tetrahedra | [SiO 4 ] 4− | olivine |
Sorosilikati | tetrahedra mara mbili | [Si 2 O 7 ] 6− | epidote, kikundi cha melilite |
Saiklosilikati | pete | [Si n O 3 n ] 2 n - | kikundi cha tourmaline |
Inosilikati | mnyororo mmoja | [Si n O 3 n ] 2 n - | kikundi cha pyroxene |
Inosilikati | mnyororo mara mbili | [Si 4 n O 11 n ] 6 n - | kikundi cha amphibole |
Filosilikati | shuka | [Si 2 n O 5 n ] 2 n - | mica na clay |
Tektosilikati | Mfumo wa 3D | [Al x Si y O (2 x +2 y ) ] x - | shondo, feldspars, zeolites |
MarejeoEdit
- ↑ Mineral - Silicates. britannica.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 25 October 2017. Iliwekwa mnamo 8 May 2018.
- ↑ Deer, W.A. (1992). An introduction to the rock-forming minerals, 2nd, London: Longman. ISBN 0-582-30094-0.
- ↑ Hurlbut, Cornelius S. (1985). Manual of Mineralogy, 20th, Wiley. ISBN 0-47180580-7.
Viungo vya njeEdit
- media kuhusu Silikati pa Wikimedia Commons
- Mindat.org, Uainishaji wa Dana
- Webmineral : Uainishaji mpya wa Dana
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Madini silikati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |