Madrid ni mji mkuu wa Hispania pia mji mkubwa wa nchi wenye wakazi 3,129,600 na pamoja na rundiko la mji milioni 5.8.

Plaza de España, Madrid
Kanisa la Almudena

Jiografia

hariri

Madrid iko katikati ya Hispania katika nyanda za juu za Castilia kwenye kimo cha m 667 m juu ya UB. Mto mdogo Manzanares unapita mjini. Kaskazini ya mji kuna milima ya Sierra de Guadarrama inayofikia kimo cha m 2,429.

Historia

hariri

Chanzo cha Madrid ni katika zamani za Waroma katika Hispania. Utawala wa Waarabu uliacha kijiji mahali pake kilichotwaliwa na mfalme Alfonso VI. wa Kastilia kikateuliwa kuwa mji mkuu wa ufalme wa Hispania mwaka 1561. Hispania ilikuwa nchi tajiri ya Ulaya wakati ule kutokana na dhahabu na fedha za koloni zake huko Amerika ya Kusini na utajiri huu uliwezesha wafalme kupamba mji kwa majengo mengi makubwa na mazuri.

Wakati wa Napoleoni Madrid ilitwaliwa na jeshi la Ufaransa lakini uasi wa wakazi wa mji ulianzisha vita ya ukombozi wa Hispania. Mji ulianza kukua katika karne ya 19 na zaidi katika karne ya 20 ukawa pia kitovu cha kiuchumi cha Hispania.

Madrid ilikuwa kitovu cha mapinduzi ya Hispania kama vile kupinduliwa kwa utawala wa kifalme na tangazo la jamhuru mwaka 1873, kuanzishwa kwa udikteta wa jenerali Miguel Primo de Rivera 1923, kutnagzawa kwa jamhuri ya pili 1931. Katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Hispania kati ya 1936 hadi 1939 mji uliharibiwa vibaya.

Picha za Madrid

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Madrid kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.