Alfabeti ya Kilatini
Aa Bb Cc Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz
(Kwa matumizi ya Kiswahili)
ch dh gh kh
mb mv nd ng ng' nj
ny nz sh th

M ni herufi ya 13 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Mi ya alfabeti ya Kigiriki.

Maana za M

hariri

Historia ya alama M

hariri
Kisemiti asilia:
picha ya maji
Kifinisia:
Mem kwa "M"
Kigiriki
Mi
Kietruski
M
Kilatini
M
         

Asili ya herufi M ni katika miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki waliipokea kutoka Wafinisia.

Wafinisia walikuwa na alama ya "Mem" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya maji wakitumia alama tu kwa sauti ya "m" na kuiita kwa neno lao kwa maji "mem". Kwa kurahisisha kazi ya kuandika waliongeza mstari mrefu upande walipoanza kuandika.

Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "Mi" bila kujali maana asilia ya "maji", ilikuwa sauti tu ya "m". Waligeuza alama kulingana na mwendo wao wa kuandika kuanzia upande wa kushoto na kufikia umbo lililokaa hivyo.

Waitalia wa kwanza wakaipokea ilivyo hata kama walirudia mara nyingi umbo la awali.

Waroma wakaendeleza alama hiyo katika alfabeti yao kwa maana hiyohiyo.

  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu M kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.