Magret Hamisi Nzomiya (alizaliwa mnamo 1987) ni mwigizaji wa filamu nchini Tanzania.

Magret Hamisi

Alizaliwa katika familia ya Wazanaki ambao ni Wakristo akapata elimu ya msingi kwenye shule ya Nyakato mkoani Mara.

Sanaa alianza toka alivyokuwa shule ya msingi, baada ya kumaliza shule alijiunga na vikundi mbali mbali vya sanaa, lakini hakubahatika kupata kikundi chenye msimamo. Mwaka 2008 alijiunga na kikundi cha Alwatan Artist Theatre chenye maskani yake Ilala. Alifaniwa majaribio na kuweza kupata nafasi ya kucheza sinema ya Bunge la wachawi. Katika sinema hiyo amecheza kama msichana mchawi anayeshirikiana na mama yake kuwafanyia ukatili mandondocha anayofuga mama yake.

Anasema kwa upande wa wasanii wa Tanzania anavutiwa muigizaji Mwajuma Abdul maarufu kama Maimuna.aliyecheza sinema ya uwanja wa dhambi. Kwa upande wa waigizaji wa nje ya Tanzania anavutiwa na Maria Clara anayecheza tamthilia ya Secret Diamor. Lengo ni kuwa msanii maarufu wa kimataifa. Anachukizwa na vitendo vya majungu, ugomvi, ubinafsi na umalaya vinavyofanywa na baadhi ya wasanii.

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Magret Hamisi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.