Maiduguri ni mji mkuu wa jimbo la Borno nchini Nigeria.

Mahali pa Maiduguri katika Nigeria
Wakimbizi wa Nigeria huko Maiduguri mnamo Agosti 2016.
Wakimbizi wa Nigeria huko Maiduguri mnamo Agosti 2016.

Mji ulianzishwa mwaka 1907 na Waingereza kama kituo cha kijeshi.

Leo hii kuna wakazi 2,000,000. Kuna Chuo Kikuu, hospitali, masoko, uwanja wa kimataifa wa ndege. Tangu 1974 reli ya Nigeria imefika mjini.

Miaka ya nyuma palikuwa na fitina kati ya Wakristo na Waislamu mjini. Waislamu ni wengi mjini penyewe na upande wa kaskazini ya Borno; Wakristo huwa wengi upande wa kusini. Hasa baada ya habari za machoro ya Mtume Muhamad huko Denmark kufika Borno yalitokea mashambulio ya vijana Waislamu dhidi ya Wakristo.

Makala hii kuhusu maeneo ya Nigeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Maiduguri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.