Majadiliano:ANC

Latest comment: miaka 17 iliyopita by Muddyb Blast Producer in topic Ubaguzi wa rangi - Apartheid

Ubaguzi wa rangi - Apartheid

hariri

Nimetumia neno "Apartheid" kwa siasa ya zamani ya Afrika Kusini. Muddy amebadilisha neno akaandika "ubaguzi wa rangi". Najua hii ni lugha ya kawaida kwa Kiswahili. Hata hivyo naona ya kwamba tunahitaji maneno ya ziada kwa sababu kuna aina nyingi za ubaguzi wa rangi. Labda tofauti hizi hazikujadiliwa sana kwa Kiswahili.

Ila tu: kama mtu mwenye asili ya Kichina abaguliwa katika Malaysia; kama Wahindi wanabaguliwa na kudharauliwa katika Uarabuni; kama Mwafrika anashambuliwa na wahuni huko Urusi; kama mtu mweupe anapigwa na vijana Wamerika weusi akiingia katika mtaa mweusi - haya yote ni ubaguzi wa rangi.

Lakini ni hali tofauti sana na siasa ile ya Afrika Kusini inayojulikana kimataifa kwa jina la la Kiafrikaans kama "apartheid". Kwa hiyo nitahitaji neno hili nikiendelea kuandika kuhusu Afrika Kusini. Je labda tuweke (ubaguzi wa rangi) kwa mabano pale ambako neno latajwa mara ya kwanza katika makala pamoja na kiungo kwenda makala ya Apartheid? --Kipala 18:47, 13 Novemba 2007 (UTC)Reply


Si vibaya. Ila tu kila kitu kinatakiwa kiwe kinaelezwa!! Hapo awali nilikuwa najua maana ya Apartheid ni ubaguzi wa rangi, kumbe inamaana nyingine nyingi tu tofauti tu. Basi haina tatizo ni vyema kuwekana sawa!--Mwanaharakati 06:51, 19 Desemba 2007 (UTC)Reply

Rudi kwenye ukurasa wa " ANC ".