Kiafrikaans

Kiafrikana (Afrikaans) ni lugha ya Afrika Kusini iliyotokea katika karne nne zilizopita kwenye msingi wa Kiholanzi pamoja na athari za lugha mbalimbali. Hata kama ni lugha iliyozaliwa Afrika kitaalamu ni kati ya lugha za Kigermanik.

Majimbo ya Afrika Kusini yenye wasemaji wengi au wengi kidogo wa Kiafrikana kama lugha ya kwanza

Imekuwa lugha rasmi katika Afrika Kusini tangu mwaka 1925 badala ya Kiholanzi. Hadi sasa ni lugha rasmi mojawapo Afrika Kusini pamoja na lugha 9 nyingine. Ni pia kati ya lugha za taifa huko Namibia.

Kiafrikana ina wasemaji wa lugha ya kwanza milioni saba na milioni kumi wasemaji kama lugha ya pili.

Kiasili kimetokea kama lugha ya makaburu ya Afrika Kusini lakini imekuwa pia lugha ya wakazi chotara katika jimbo la Rasi Magharibi ("Cape Coloureds"). Leo hii wasemaji wa asili ya Ulaya ni chini ya nusu ya wasemaji wote wa Kiafrikana.

Inatumika pia Botswana, Eswatini na Zimbabwe.

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiafrikaans kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.