Majadiliano:Abdulrazak Gurnah

Latest comment: miaka 2 iliyopita by Kipala in topic Mtanzania, Mwingereza, Mzanzibari ?

Mtanzania, Mwingereza, Mzanzibari ? hariri

Je ni kweli sahihi kumwita "Mtanzania"? Aliishi kama raia wa Zanzibar kwa miaka 15 hadi 1964, alikuwa Mtanzania miaka 3 halafu alikimbia (sijakuta bado maelezo kuhusu hali yake wakati ule; kwa nini anatajwa kama mkimbizi?; familia yake ni watu walioitwa wakati ule "Waarabu"; wengi wao waliuawa 1964 wengine kufukuzwa au kuteswa kwa namna mbalimbali; sijasikia kwamba anaongea Kiarabu, Kiswahili chake ni cha kifasaha). Halafu tangu miaka 50 hivi anaishi Uingereza ni raia huko. Tumwitaje? Kama angekuja tanzania, asingeweza kujenga nyumba yake - isipokuwa katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwa wageni huko Unguja. Kipala (majadiliano) 12:24, 8 Oktoba 2021 (UTC)Reply

Return to "Abdulrazak Gurnah" page.