Majadiliano:Chomboanga
Latest comment: miaka 9 iliyopita by Kipala in topic Chombohewa ?
Chombohewa ?
haririChaguo la jina la makala (kwa "aircraft") kilifuata kamusi ya KAST. Jinsi ilivyo mara nyingi, pendekezo hili la KAST halikupokelewa katika lugha. Ilhali nakuta zaidi "chomboanga" kwa vyombo vya anga la nje najiuliza kama afadhali makala ihamishwe kwenda "chombohewa".
Je kuna uwezekano ya kwamba hii ingeeleweka kuwa chombo cha kutunza au kufunga hewa?
Kama ni vile, labda afadhali "chombo cha usafiri wa hewani". Hili ni jina ndefu lakini kwa kawaida hatujadili sana vyombo hivi vyote kwa pamoja (eropleni, helikopta, purutangi, roketi...), na kwa matumizi ya kiteknolojia inaweza kufaa pia. Wenzangu wanaonaje? Kipala (majadiliano) 14:25, 24 Agosti 2015 (UTC)