Majadiliano:Itikadi kali
Latest comment: miaka 7 iliyopita by Muddyb Blast Producer
Makala imetaja mifano ya kidini, lakini ni Ukristo tu, lakini ukisoma Wikipedia ya Kiingereza wameweka dini zote.. Kama ni kuweka mifano ya dini, bora uweke yote na si moja. Matokeo yake nilidhani makala hii ni ya dini, kumbe ni kuhusu FUNDAMENTALIZIM! Wazo tu..--MwanaharakatiLonga 12:08, 30 Januari 2017 (UTC)
- Dunia kweli uwanja wa fujo. Nimeona Uislamu unavyotumiwa vibaya katika dunia hii ya sasa. Haya, ile ya Marekani kuvamia Libya na kumuua kiongozi wake tuite FUNDAMENTALIZIMU nayo? Maana hakuna tofauti na Ugaidi..--MwanaharakatiLonga 12:32, 1 Februari 2017 (UTC)
- Ndugu, nilipotunga ukurasa huu nilikwepa kuzungumzia Uislamu kwa sababu ya kulinda amani kwanza kati yetu. Sasa kwa kuwa umeomba mwenyewe nimeongeza juu yake na juu ya Uhindu, kwa sababu wenye itikadi kali wako kila mahali. Kuhusu Marekani na maovu yake mengi, si suala la dini, ni suala la siasa na hatimaye ya uchumi tu. Kaulimbiu yao ni "In Go(l)d we trust"! Nadhani ni kitu cha namna hiyo pia kwa DAESH na kesi nyingine nyingi za kusikitisha. Muhimu ni kulea vizazi vipya kuheshimiana, si kubaguana, kama tunavyojaribu kufanya katika shule hii. Amani kwa wote! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:01, 1 Februari 2017 (UTC)
- Mkuu Riccardo, usitoe macho! Ni mtazamo tu. Walau nimejua nini kinachopelekea Marekani kutangaza vita na Uislamu na nchi zake, kumbe ni mali. Samahani kuku-kwa-za.. Haikuwa maana yangu. Samahani sana, tena sana na sana! Niseme kwa kinyumbani kwenu ili kusisitiza: "Quando qualcuno chiede il perdono, non prendere troppo tempo per accettare la sua / sue scuse!".--MwanaharakatiLonga 04:39, 2 Februari 2017 (UTC)