Majadiliano:Mfumo wa Jua

(Elekezwa kutoka Majadiliano:Mfumo wa jua)
Latest comment: siku 13 zilizopita by Riccardo Riccioni in topic Ruhusa ya kuhariri

Atlasi yangu ya shule, pamoja na tovuti hii vinataja Utaridi = Pluto ("sayari" ya tisa). Matt Crypto 22:56, 12 Februari 2006 (UTC)Reply

Kumbe!! Nimeangalia [1]. Utaridi namna gani Pluto?? Pluto imejulikana tangu 1930 - pia kamusi Kiing-Kisw ya TUKI inatumia "Pluto". Lakini sishangai sana. Vitabu vya shule vya TZ... Ningeweka pesa kiasi kwa etimolojia yangu. Naona ingekuwa vema kumpata mtu katika TUKI huko DSM. Nimepata Utaridi katika kijitabu cha "Maajabu ya Ulimwengu" (kimetungwa na P. Sebald OSB, Benedictine Publications Ndanda-Peramiho 1985). Hata yeye anabadilishabadilisha Utaridi na Zebaki akitaja sayari ya kwanza. Lakini Pluto ni Pluto, hakuna njia kutumia jina la Kiarabu wakati Waarabu wenyewe hawana jina na kutumia lile la Kigiriki kipya, tena Utaridi inajulikana kabisa kuwa sayari ya kwanza??

Hata nisingeshangaa kama mtu amechanganya kila kitu ikawa utaratibu sasa. Kwa upande mwingine hadi sasa si watu wengi sana wanaotaja sayari kwa majina ya Kiswahili. Kwa hiyo itakuwa ajabu kwa wanahistoria ya lugha lakini haigusu watu wengi bado. Hata kuna uwezekano ya kwamba mkono mmoja (TUKI kamusi kiing-kisw) unasema kitu kimoja, halafu mkono mwingine (k.km. BAKITA au wizara ya elimu) unasema tofauti ilhali hawajui. Naona tuweke tuangalie watu wanasemaje tukusanye maoni kidogo. --Kipala 02:07, 13 Februari 2006 (UTC)Reply

Marekebisho kidogo: sayari ya Zuhura si Zebaki. Zebaki ni madini yanayoitwa Mercury katika lugha ya kiingereza, ambayo ni sayari ya Zebaki

Ruhusa ya kuhariri

hariri

@Muddyb @Riccardo Riccioni wakabidhi tu wana ruhusa ya kuhariri makala hii. lakini, hata katika wikipedia ya kiingereza na wikipedia nyingine kubwa, mara chache wanaweka vizuio kama hizi. mngeweza kukiondosha kizuio ili niweze kuichangia makala? Kisare (majadiliano) 11:33, 22 Desemba 2024 (UTC)Reply

@Kisare nadhani Muddyb anaweza kufanya hivyo. Mimi natarajia kujiuzulu kama ulivyotaka. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:23, 22 Desemba 2024 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Mfumo wa Jua ".