Majadiliano:Misimu (lugha)

Latest comment: miezi 6 iliyopita by 197.237.69.223

Niangalia kamusi sanifu za Tuki na Bakita, neno ni "simo" lakini si "msimu", ingawa Tuki-ESD naona pia "misimu" kama kisawe cha simo. Naona kwa Sacleux kwamba maana asilia ya simo ilikuwa "jambo jipya". Kwa hiyo, kama inatumwa sasa kwa lugha, kwa maana ya "maneno mapya". Nikitumia upekuzi wa google, napata pia "misimu":

"Misimu ni jumla ya maneno yote ambayo siyo sanifu katika lugha yoyote mathalani Kiswahili ambayo yameibuliwa na vikundi vidogo vya watu wenye utamaduni unaofanana kwa lengo la kuwa na usemi mmoja unaolinda, mawazo na mawasiliano vya wanavikundi. Sababu ya kuitwa misimu ni kuwa maneno hayo huzuka na kupotea na mara nyingi kulingana na matukio fulani katika jamii husika." (Chanzo: Swahilihub). Kwa hiyo nitahamisha lemma na kurudisha maelezo yaliyofutwa. Kipala (majadiliano) 08:58, 27 Januari 2022 (UTC)Reply

Asante sana kipala 197.237.69.223 15:06, 14 Juni 2024 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Misimu (lugha) ".